Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:07

Wananchi wa Ghana wapiga kura kuchagua rais na wabunge


Picha ya mgombea wa urais wa chama cha National Democratic Congress (NDC) na rais wa zamani wa Ghana John Dramani Mahama, Disemba 7, 2024.
Picha ya mgombea wa urais wa chama cha National Democratic Congress (NDC) na rais wa zamani wa Ghana John Dramani Mahama, Disemba 7, 2024.

Vituo vya kupigia kura katika uchaguzi wa rais na bunge nchini Ghana vimefunguliwa Jumamosi, katika uchaguzi ambao ni mtihani kwa taifa hilo la kidemokrasia ambalo lilitikiswa na machafuko mabaya na mapinduzi ya kijeshi katika miaka ya nyuma.

Watu milioni 18.7 walijiandikisha kupiga kura katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi inayokabiliwa na moja ya mizozo mibaya ya kiuchumi katika historia yake. Hata hivyo, wagombea wawili wakuu wametoa matumaini kidogo kwa ajili ya mabadiliko kwa taifa.

Ghana iliwahi kuwa mfano mzuri wa demokrasia katika kanda hiyo. Wakati ambapo mapinduzi ya kijeshi yalitishia demokrasia katika kanda ya Afrika Magharibi, Ghana imeendelea kuonekena kama nchi yenye utulivu wa kidemokrasia yenye historia ya kufanya uchaguzi wa amani.

Iliwahi pia kuwa nchi yenye uchumi ulioimarika ikijivunia maendeleo yake ya uchumi.

Lakini katika miaka ya hivi karibuni, nchi hiyo imekumbwa na mzozo mbaya wa kiuchumi, ikiwa ni pamoja mfumko mkali wa bei na ukosefu wa ajira.

Forum

XS
SM
MD
LG