Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:25

Watu watano wauawa katika shambulizi kwenye soko la Christmas Ujerumani


Watu waweka maua na mishuma kwenye eneo la shambulizi la gari kwenye soko la Christmas huko Magdeburg, Ujerumani. Disemba 21, 2024. Picha ya AFP
Watu waweka maua na mishuma kwenye eneo la shambulizi la gari kwenye soko la Christmas huko Magdeburg, Ujerumani. Disemba 21, 2024. Picha ya AFP

Wajerumani Jumamosi wameomboleza waathirika wa shambulizi lililofanywa na daktari raia wa Saudi Arabia ambaye aliendesha kwa makusudi gari lake ndani ya umati wa watu na kuwagonga wale waliokuwa kwenye soko la kuuza bidhaa za siku kuu ya Christmas, na kuua watu watano.

Watu 200 walijeruhiwa katika shambulizi hilo.

Maafisa walimkamata mtu huyo mwenye umri wa miaka 50 kwenye eneo la shambulizi katika mji wa Magdeburg Ijumaa jioni na kumuweka chini ya ulinzi ili kumuhoji.

Ameishi nchini Ujerumani kwa karibu miongo miwili, akifanya kazi ya udaktari huko Bernburg, umbali wa kilomita 40 kaskazini mwa Magdeburg, maafisa wamesema.

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz alisema watu 40 walijeruhiwa vibaya.

Vyombo vya habari kadhaa vya Ujerumani vimemtaja mshukiwa kama Taleb A na kuhifadhi jina lake jingine kulingana na sheria za kuhifadhi usiri wa mtu, na kuripoti kwamba alikuwa daktari bingwa wa magonjwa ya afya ya akili.

Hadi Jumamosi, majibu yalikuwa hayajatolewa kuhusu kilichomfanya kuelekeza gari ndani ya umati wa watu katika mji huo wa mashariki mwa Ujerumani.

Forum

XS
SM
MD
LG