Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:10

Vyama vya upinzani vya Afrika Kusini vyataka kesi dhidi ya Ramaphosa ifufuliwe


Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa .
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa .

Vyama viwili vya upinzani vya Afrika Kusini Jumanne vimeomba Mahakama ya Juu ifufue kesi ya kutokuwa na imani na Rais Cyril Ramaphosa kutokana na kashfa ya zaidi ya dola nusu milioni pesa taslimu zilizopatikana kwenye shamba lake na kisha kupotea kupitia wizi.

Chama cha The leftist Economic Freedom Fighters na kile cha Transformation Movement wameomba Mahakama ya Katiba kufutilia mbali kura ya bunge ya 2022 iliyomuokoa Ramaphosa kutokana na kura ya kutokuwa na imani naye.

Chama cha Ramaphosa cha African National Congress, ANC, kilitumia wingi wa wabunge wake kumuokoa bungeni. Vyama hivyo vya upinzani vimesema kuwa bunge halikutimiza jukumu lake la kuwajibisha rais, hata baada ya uchunguzi kuonyesha ushahidi kuwa Ramaphosa alikuwa na hatia.

ANC kilipoteza wingi wake bungeni kwenye uchaguzi wa Mei, na kwa hivyo itakuwa hatari kwa Ramaphosa iwapo kesi dhidi yake itafufuliwa. Kiongozi huyo alichaguliwa kwa muhula wa pili Juni kwa usaidizi wa vyama shirika, huku akiunda serikali ya muungano.

Vyama vilivyowasilisha ombi hilo jipya kwa mahakama hata hivyo havina wabunge wa kutosha kumuondoa Ramaphosa isipokuwa vipate uungaji mkono wa vyama vilivyojiunga kwenye serikali.

Forum

XS
SM
MD
LG