Waziri Mkuu wa Ufaransa Michael Barnier amewasilisha barua ya kujiuzulu kwake asubuhi ya leo katika makazi ya rais ya Elysee.
Hatua hii imekuja siku moja baada ya bunge la taifa kumuondoa kwa kura ya kutokuwa na imani naye ambayo imeiacha ufaransa bila ya serikali.
Rais wa ufaransa Emanuel Macron atahutubia taifa leo jioni.
Macron anatarajiwa kuzingatia zaidi kuleta utulivu katika mzozo wa kisiasa na kumteua waziri mkuu mpya.
Kura ya kutokuwa na imani naye ilipita kwa kura 331 katika bunge la taifa , hivyo kumlazimisha Barnier kujiuzulu baada ya miezi mitatu madarakani , ukionekana muda mfupi kwa waziri mkuu yoyote katika historia ya Ufaransa.
Wabunge wa Ufaransa Jumatano wamepiga kura ya kuiondoa serikali ya waziri mkuu Michel Barnier baada ya miezi mitatu tu ikiwepo madarakani, katika hatua ya kihistoria ambayo inaiweka tena nchi hiyo katika hali tete ya kisiasa.
Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 60, bunge la taifa limeindoa serikali iliyo madarakani, kwa kuidhinisha kura ya kutokuwa na imani na serikali iliyopendekezwa na chama cha mrengo mkali wa kushoto lakini ambayo iliungwa mkono na chama cha mrengo mkali wa kulia kinachoongozwa na Marine Le Pen.
Kuondolewa kwa haraka kwa waziri mkuu Barnier kwenye wadhifa wake kunajiri baada ya uchaguzi wa mapema wa bunge uliofanyika kipindi cha msimu wa kiangazi mwaka huu ambapo hakuna chama kilichopata wingi wa wabunge, huku chama cha mrengo mkali wa kulia kikiwa na mchango mkubwa ili serikali iweze kuendelea kuongoza.
Forum