Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 13, 2024 Local time: 11:32

Trump akosoa hatua ya Biden kutoa msamaha kwa mtoto wake Hunter


Rais wa Marekani Joe Biden akiwa na Rais mteule wa Marekani Donald Trump ikulu ya Marekani.
Rais wa Marekani Joe Biden akiwa na Rais mteule wa Marekani Donald Trump ikulu ya Marekani.

Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza msamaha kwa mtoto wake Hunter, ambaye angehukumiwa mwezi huu kwa makosa ya kumiliki silaha na kodi na huenda angehukumiwa kifungo cha miaka kadhaa.

Biden kwa miezi kadhaa aliahidi kutompa msamaha mtoto wake mwenye umri wa miaka 54, wakili ambaye kwa miaka kadhaa aligubikwa na tatizo la uraibu wa cocaine huku maisha yake yakididimia bila ya kudhibitiwa.

Lakini rais huyo alisema katika taarifa yake siku ya Jumapili kuwa upande wa mashtaka wa Hunter Biden walikuwa wabaguzi na ushawishi wa kisiasa, wenye lengo la kuharibu kampeni ya kuchaguliwa kwake tena kabla hajajitoa katika kinyang’anyiro hicho mwezi Julai kwa kipindi cha miaka minne mingine.

“Tuhuma hizi za kesi yake zililetwa baada tu ya wapinzani wangu wa kisiasa katika Bunge kuwachochea kunishambulia na kupinga kuchaguliwa kwangu,” alisema Biden

Hunter Biden alikutwa na makosa ya jinai matatu mwezi Juni kwa kununua bunduki mwaka 2018. Waendesha mashtaka walisema alidanganya katika fomu ya serikali kuu kuwa hatumii kinyume cha sheria au hana uraibu wa dawa za kulevya.

FILE PHOTO: FILE PHOTO: Rais Biden akiwa na mtoto wake Hunter Biden.
FILE PHOTO: FILE PHOTO: Rais Biden akiwa na mtoto wake Hunter Biden.

Pia alikiri makosa kwa mashtaka tisa ya kodi ya serikali kuu katika kesi moja ambapo alituhumiwa kushindwa kulipa kodi ya kiasi kisichopungua cha dola milioni 1.4.

Alikuwa akabiliwe na kifungo cha hadi miaka 17 katika kesi ya kodi wakati uliopangwa kusikilizwa kesi hiyo huko Los Angeles Disemba 16, ijapokuwa wataalam wa hukumu walisema kuwa ingewezekana kuwa kama mkosaji wa mara ya kwanza, angeweza kutumikia kifungo kisichozidi miezi 36.

Hunter Biden alikuwa anakabiliwa na kifungo cha juu zaidi, cha miaka 25, katika kesi ya bunduki lakini ingewezekana zaidi, kutokana na kuwepo kuhumu kadhaa za kesi kama hiyo, kupewa hukumu ya muda mfupi zaidi, pengine ya hadi miezi 16 wakati kesi iliyopangwa kusikilizwa huko Delware Disemba 13.

Hatua ya rais aliyoichukua Jumapili kutoa msamaha kwa Hunter Biden katika kesi zote mbili, na pia kwa kosa lolote jingine ambalo “ametenda au alitenda au alishiriki” kuanzia Jan 1, 2014 hadi Jan 1, 2024.

Hunter Biden alisema katika taarifa hiyo, “Nimekiri na kuwajibika kwa makosa yangu wakati wa siku nyeusi za uraibu wangu – makosa ambayo yametumiwa kunidhalilisha kwa umma na kunifedhehesha mimi na familia yangu kwa maslahi ya kisiasa.”

Rais huyo alisema katika taarifa yake kuwa anatarajia “Wamarekani wataelewa kwa nini baba na rais angefikia uamuzi huu.”

“Katika kipindi changu chote cha kazi yangu nimefuata msingi ufuatao: Waambie watu wa Marekani ukweli. Watakuwa ni waadilifu katika kufikiria kwao.

Huu ndiyo ukweli: Nina amini katika mfumo wa sheria, lakini kadiri nilivyopambana nalo, pia naamini siasa chafu zimechafua mchakato huu na zimepelekea ukiukwaji wa sheria – na mara nilipofanya uamuzi huu wikiendi hii, ilikuwa hakuna maana ya kuchelewesha jambo hili zaidi,” Biden alisema.

Rais mteule Donald Trump aliikosoa hatua hiyo, akiita “kutumia sheria vibaya” ukilinganisha na mamia ya wafuasi wa Trump ambao wamefungwa baada ya kukutwa na hatia kwa makosa mbalimbali yakitokana na ghasia katika Bunge la Marekani Januari 6, 2021, wakati wakijaribu kulizuia Bunge kuidhinisha kuwa Biden alimshinda Trump katika kinyang’anyiro cha kuchaguliwa tena katika kampeni ya 2020.

Trump amesema kuwa atafikiria kutoa msamaha kwa wengi kati ya wale waliovamia bunge atapochukua madaraka tena Januari 20 baada ya kushinda uchaguzi wa urais mwezi Novemba, wakati kesi nyingine bado hazijasikilizwa.

Trump, katika kipindi cha mwisho wa awamu yake ya kwanza ya urais, alitoa msamaha kwa Charles Kushner, baba mkwewe Jared Kushner, ambaye alikutwa na makosa ya kodi na mashtaka mengine. Siku ya Jumamosi, Trump alisema anakusudia kumchagua Kushner baba kuwa balozi wa Marekani nchini Ufaransa.

FILE - Charles Kushner
FILE - Charles Kushner

Trump pia ametoa msamaha kwa mmoja wa washauri wake wa usalama wa taifa wa zamani, Michael Flynn, meneja wa kampeni wa zamani Paul Manafort, mkuu wa mikakati wa zamani Steve Bannon na msaidizi wa kampeni George Papadopoulos, kati ya wengine.

Hisia tofauti kuhusu Rais Biden kutoa msamaha kwa mtoto wake zilitofautiana kote katika medani za kisiasa nchini Marekani na siyo kawaida kuweza kutabirika katika misimamo ya kisiasa kama ilivyo wakati yanapotangazwa maamuzi yenye mvutano.

Chuck Grassley, seneta Mrepublikan kutoka Iowa, alibandika katika mtandao wa X ujumbe kuwa “amestushwa” na msamaha huo kwa sababu Biden baba “ alisema mara nyingi sana kuwa hatofanya hivyo na nilimuamini. Ni aibu kwangu.”

Lakini Eric Holder, Mdemokrat ambaye alikuwa mwanasheria mkuu wa Marekani chini ya utawala wa rais wa zamani Barack Obama, alisema mtoto wa ais ameshitakiwa tu kwa sababu ya ubini wake wa Biden.

Hakuna mwanasheria wa Marekani “ aliyewahi kufungua kesi kama hii kwa vielelezo vilivyoambatana na kesi hii.”

Forum

XS
SM
MD
LG