Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 18:50

Mike Pence atoa shutma dhidi ya rais wa zamani Donald Trump


Makamu wa Rais wa zamani Mike Pence alipozungumza katika Maktaba ya Rais ya Ronald Reagan na Makumbusho Novemba 17, 2022. AP
Makamu wa Rais wa zamani Mike Pence alipozungumza katika Maktaba ya Rais ya Ronald Reagan na Makumbusho Novemba 17, 2022. AP

Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Marekani, Mike Pence, anayetarajiwa kuwania uteuzi wa urais wa chama cha Republican mwaka wa 2024, ametoa shutma kali dhidi ya rais aliyemtumikia kwa uaminifu, Donald Trump.

Pence alisema Trump alihusika binafsi kuhimiza ghasia za Januari 6, 2021, za wafuasi wake katika Bunge la Marekani, kujaribu kuzuia Bunge hilo kuthibitisha kwamba Joe Biden alimshinda rais wa 45 katika uchaguzi wa mwaka 2020.

“Rais Trump alikosea, sikuwa na haki ya kutengua uchaguzi,” Pence aliambia kundi la waandishi wa habari waandamizi wa mjini Washington na maafisa wa serikali katika mlo wa jioni wa kila mwaka wa Gridiron Jumamosi usiku. "Na maneno yake ya kutojali yalihatarisha familia yangu na kila mtu katika bunge siku hiyo. Na najua historia itamfanya Donald Trump kuwajibika.

Wiki iliyopita Pence alimwomba jaji azuie wito wa kutoa ushahidi wake mbele ya mahakama kuu inayochunguza uasi huo na juhudi za Trump za kuhalalisha matokeo ya uchaguzi. Lakini wakati wa chakula cha jioni, alitupilia mbali majaribio yanayoendelea, haswa na wabunge wa kihafidhina na wachambuzi wa Fox News, kupuuzia habari za ghasia katika bunge ambapo zaidi ya wafuasi 1,000 wa Trump wamekamatwa na karibu nusu hadi sasa wametiwa hatiani kwa makosa mengi.

XS
SM
MD
LG