Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 28, 2025 Local time: 05:49

Trump ndiye rais mteule wa Marekani 2024


Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump na mkewe, Melania Trump katika ukumbi wa mikutano wa Palm Beach, kaunti ya West Palm Beach, Florida.
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump na mkewe, Melania Trump katika ukumbi wa mikutano wa Palm Beach, kaunti ya West Palm Beach, Florida.

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump alichaguliwa kuwa rais wa 47 mapema Jumatano baada ya kushinda katika majimbo kadhaa muhimu, yakiwemo Pennsylvania na Wisconsin, akimshinda Makamu wa Rais Kamala Harris. 

Kufikia mwendo wa saa kumi na mbili alfajiri saa za Washington DC, Trump alikuwa akiongoza kwa kura 277 za wajumbe huku Harris akiwa na 224.

Awali, Trump alipata ushindi katika majimbo yaliyokuwa na ushindani mkubwa ya Pennsylvania, Georgia na North Carolina na kumpa angalau kura 267 kati ya kura 270 zinazohitajika kupata kupata ushindi.

Harris angehitaji kushinda majimbo yote hayo, pamoja na Michigan, Wisconsin, Nevada na Arizona.

Trump alidai ushindi mapema Jumatano alipokuwa akiwashukuru wafuasi wake katika mkutano wa hadhara huko Florida.

Aidha, Warepublican walichukua udhibiti katika Seneti yenye wanachama 100 mwishoni mwa Jumanne, lakini bado haijajulikana ni chama kipi kingedhibiti baraza la wawakilishi.

Habari zaidi zitafuata......

Forum

XS
SM
MD
LG