Kabla ya kuanza safari yao kuelekea upande wa kaskazini, wahamiaji hao walikusanyika Tapachula, ambao ni mji mkuu wa jimbo la kusini mwa Mexico la Chiapas, wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe kama, “ “Hakuna tena damu ya wahamiaji,” pamoja na picha za Bikra wa Guadalupe, ambaye ana umuhimu mkubwa wa kidini na kitamaduni miongoni mwa wakazi wa Mexico, kulingana na shirika la habari la Reuters.
“ Tunataka serikali ya Marekani ituangalie, na ituone kama watu wanaotaka kufanya kazi ,na wala siyo kumuumiza yeyote,” Roy Murillo mhamiaji kutoka Honduras aliyejiunga kwenye msafara huo akiwa na watoto wake wawili na mke wake mjamzito, alisikika akisema. Katika miaka ya karibuni, misafara yenye watu wanaolenga kuingia Marekani imekuwa ikiwasili kwenye mpaka wa Mexico na Marekani, mara nyingi wakitembea pamoja kwa makundi kwa ajili ya usalama.
Mji wa Tapachula ambao hupitiwa na maelfu ya wahamiaji, katika miezi ya karibuni umekuwa mmoja ya miji hatari nchini Mexico, ambako magenge hushambulia wahamiaji.
Forum