Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 11:12

Wamarekani wanapiga kura kumchagua rais ajaye nchini humo


Wagombea urais Marekani, Makamu Rais Kamala Harris (L) na Rais wa zamani Donald Trump.
Wagombea urais Marekani, Makamu Rais Kamala Harris (L) na Rais wa zamani Donald Trump.

Wagombea wote wawili walifanya kampeni Jumatatu huko Pennsylvania, moja ya majimbo yaliyotazamwa kwa karibu.

Mamilioni ya wapiga kura nchini Marekani wanatarajiwa kupiga kura leo Jumanne wataamua iwapo makamu rais Kamala Harris au rais wa zamani Donald Trump atakuwa kiongozi mpya wa nchi hiyo.

Kura zinazoelekea siku ya uchaguzi zilionyesha kinyang’anyiro kikali, hasa katika majimbo kadhaa yenye ushindani mkubwa ambayo yatakuwa muhimu katika kuamua mshindi.

Wagombea wote wawili walifanya kampeni Jumatatu huko Pennsylvania, moja ya majimbo yaliyotazamwa kwa karibu, wakifanya mfululizo wa mikutano ya hadhara iliyokuwa katika maeneo yanayokaribiana na kila mmoja, katika mji wa Pittsburgh huku wakionyesha imani ya ushindi katika kampeni zao wenyewe.

Forum

XS
SM
MD
LG