Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 04:31

Kamala akubali kushindwa na kumpongeza Trump


Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris, Jumatano amekubali kushindwa katika uchaguzi wa urais, akimpigia simu Rais wa zamani Donald Trump, kumpongeza kwa ushindi wake na kuwaambia wafuasi wake kwamba si wakati wa kumaliza vita vya kutetea maono ya kimaendeleo kwa nchi hiyo.

“Ni sawa kusikia huzuni na kukata tamaa,” aliuambia umati wa watu katika Chuo Kikuu cha Howard, hapa Washington, chuo alicho somea.

Mgombea huyo wa chama cha Demokrat amesema mapambano yataendelea katika kura, mahakamani na majukwaa ya umma. Trump ameshinda uchaguzi wa Jumanne na kuwa rais wa 47 wa nchi hiyo huku akitwaa takriban majimbo matano kati ya saba muhimu ya ushindani na alikuwa akiongoza katika mengine mawili wakati hesabu za kura zikiendelea.

Trump na makamu wake JD Vance, wataingia madarakani Januari 20 kwa muhula wa miaka minne.

Forum

XS
SM
MD
LG