Ameahidi kukabidhi madaraka kwa Trump, ambaye anachukua hatamu za uongozi, ambaye aliwashawishi wafuasi wake kuandamana hadi kwenye jengo la bunge wakati wajumbe walipokuwa wanarasimisha ushindi wa Biden 2020.
Rais Joe Biden jana Alhamisi aliahidi kukifanya kipindi cha mpito cha mrithi wake Rais mteule Donald Trump kuwa na utaratibu mzuri. Pia ameomba umoja baada ya kushindwa kwa mgombea aliyempendelea, Makamu Rais Kamala Harris.
Joe Biden, Rais wa Marekani: “Watu wamepiga kura na kuchagua viongozi wao, na walifanya hivyo kwa amani. Sisi tuko katika demokrasia, nia ya watu siku zote ndiyo inashinda.”
Trump, katika hotuba yake ya ushindi siku moja kabla, pia alisisitiza umoja, wakati akielezea njia ya wazi miongoni mwa wapiga ambayo imempa yeye ushindi mzuri.
Donald Trump, Rais Mteule alisema: “Walitoka kila upande: umoja wafanyakazi, wale ambao hawako katika umoja huo, Wamarekani wenye asili ya Kiafrika, Wamarekani wa Kispanish, Wamarekani wa Asia, Waarabu, Waislamu. Tulikuwa na kila mtu. Ilikuwa vizuri sana. Yalikuwa marekebisho ya kihistoria, kuwaunganisha raia kutoka kila upande katika jambo moja muhimu.”
Miaka minne ya awali, Trump alikataa kukubali kuwa alishindwa na Biden. Alisimama kimya wakati umati uliokuwa na hasira wa wafuasi wake walipovamia jengo la Bunge la Marekani wakati mchakato wa kurasmisha matokeo ukiendelea hapo Januari 6, 2021. Biden jana alifanya jambo tofauti.
Joe Biden, Rais wa Marekani alieleza: “Tunakubali uchaguzi uliofanya na nchi. Nimesema mara nyingi, huwezi kuipenda nchi yako pale tu unaposhinda. Huwezi kumpenda jirani yako pale tu mnapokubaliana.”
Biden pia alisema alitumaini hakutakuwa na maswali kuhusu uadilifu wa mfumo wa uchaguzi Marekani.
Joe Biden, Rais wa Marekani anasema: “Ni uaminifu. Ni haki, na ni uwazi. Unaweza kuaminiwa, iwe umeshinda au umeshindwa.”
Kuapishwa kwa Trump kwa mara ya pili kutafanyika Januari 20, 2025.
Forum