Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 03, 2024 Local time: 20:13

Trump amteua mkuu wa wafanyakazi White House


Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, amemteua Susie Wiles, aliyekuwa meneja wa kampeni yake ya ushindi, kuwa mkuu wa wafanyikazi wa White House, na kuwa mwanamke wa kwanza kushikilia nafasi hiyo yenye ushawishi.

Wiles anasifiwa sana ndani na nje ya watu wa karibu wa Trump kwa kuendesha kile ambacho kinaelezewa kuwa kampeni ya kimkakati wa hali ya juu na kufanya vyema.

Toka awali alionekana kuwa mshindani mkuu wa nafasi hiyo muhimu ya White House. Kwa kiasi kikubwa aliepuka kujitokeza hadharani hata kukataa kuzungumza wakati Rais mteule Trump alipokuwa akisherehekea ushindi wake Jumatano asubuhi.

Alikataa cheo rasmi cha meneja wa kampeni, akikwepa kulengwa kutokana na historia ya Rais mteule Trump kwa watu waliochukuwa jukumu hilo.

Kuchaguliwa kwa Wiles ni uamuzi wa kwanza wa Trump, na ambao unaweza kuelezea namna utawala wake ujao utakavyokuwa.

Forum

XS
SM
MD
LG