Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:01

Waliovamia bunge la Marekani kuhukumiwa


Wanachama wa Proud Boys kiungana na wafuasi wa rais wa Marekani Donald Trump wakati wa mkutano wa hadhara huko Washington, DC, Novemba 14, 2020. Picha na Andrew CABALLERO-REYNOLDS / AFP.
Wanachama wa Proud Boys kiungana na wafuasi wa rais wa Marekani Donald Trump wakati wa mkutano wa hadhara huko Washington, DC, Novemba 14, 2020. Picha na Andrew CABALLERO-REYNOLDS / AFP.

Jaji wa serikali kuu nchini Marekani atawahukumu wanachama wengine wawili wa kundi lenye msimamo wa mrengo wa kulia Proud Boys siku ya Ijumaa.

Wanachama hao ambao walivamia bunge la Marekani Januari 6, 2021, katika jitihada ambayo haikufanikiwa za wafuasi wa rais aliyekuwa madarakani wakati huo Donald Trump za kutaka kulizuia bunge la Marekani kurasmisha ushindi wa Rais Joe Biden katika uchaguzi.

Mshitakiwa wa kwanza wa Proud Boy ambaye atahukumiwa Ijumaa asubuhi ni Dominic Pezzola, hakuwa na jukumu la uongozi katika kundi hilo na alikuwa mshtakiwa pekee kati ya watano ambaye hakupatikana na hatia ya kushiriki katika njama za uchochezo huo. Pezzola alitiwa hatiani kwa makosa mengine ikiwa ni pamoja na kuingilia kati shughuli rasmi na kuwashambulia polisi. Mshtakiwa wa pili, Ethan Nordean, alikuwa kiongozi wa kundi hilo ambaye alikutwa na hatia za kula njama za uchochezi na uhalifu mwingine.

Maelfu ya wafuasi wa Trump walilishambulia jengo la Bunge (Capitol) kufuatia hotuba ambayo chama cha Republican kilitoa tuhuma za uongo kwamba kushindwa kwake katika uchaguzi wa Novemba 2020 kulitokana na udanganyifu ulioenea.

Trump ameendelea kutoa madai hayo ya uongo hata wakati akiongoza katika kinyang'anyiro cha chama cha Republican kuwania uteuzi wa kugombea urais wa 2024 kutoa changamoto kwa rais Biden wa chama cha Democrat.

Watu watano akiwemo afisa wa polisi walifariki wakati au muda mfupi baada ya ghasia hizo, na zaidi ya maafisa 140 wa polisi kujeruhiwa. Capitol ilipata uharibifu wa mamilioni ya dola.

Hukumu ya Pezzola na Nordean inafuatia amri ya jaji wa Wilaya wa Marekani Timothy Kelly siku ya Alhamisi kuamuru viongozi wengine wawili wa zamani wa Proud Boys, Joseph Biggs kutumikia kifungo cha miaka 17 jela na Zachary Rehl ambaye naye atatumikia kifungo cha miaka 15.

Serikali inataka Pezzola ahukumiwe kifungo cha miaka 20 jela, na kifungo cha miaka 27 kwa Nordean.

Ingawa Pezzola hakupatikana na hatia ya uchochezi, waendesha mashtaka walisema shambulio lake kwa afisa wa polisi wa zamani wa Capitol Mark Ode, ambapo aliiba ngao ya afisa huyo wa polisi ya kutuliza ghasia na kuitumia kuvunja dirisha la Capitol, kitendo ambacho kinasaidia kuhalalisha kifungo cha muda mrefu gerezani.

Chanzo cha bahari hii ni Shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG