Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 14:46

Warepublikan wakabiliana katika mdahalo wa kwanza kwelekea uchaguzi wa rais, Trump aususia


Mdahalo wa wawaniaji wa tikiti ya chama cha Republikan ili kugombea urais wafanyika mjini Milwauke, Wisconsin.
Mdahalo wa wawaniaji wa tikiti ya chama cha Republikan ili kugombea urais wafanyika mjini Milwauke, Wisconsin.

Wanasiasa wanaowania nafasi ya kugombea urais wa Marekani kwa tikiti ya chama cha Republikan walikabiliana kwa maneno makali wakati wa mdahalo wa kwanza wa msimu huu wa uchaguzi uliofanyika mjini Milwauke, Wisconsin, Jumatano usiku, ulioongozwa na shirika la habari la Fox News.

Lilikuwa ni tukio kubwa katika kalenda ya siasa za Marekani ambapo wagombea tisa walikuwa wamefuzu kushiriki mdahalo huo katika ukumbi wa Fiserv, kulingana na kanuni za Chama cha Republican.

Hata hivyo, mwaniaji anayeongoza katika tafiti za maoni - Rais wa zamani Donald Trump – hakushiriki hafla hiyo.

Makamu wa rais wa zamani Mike Pence ni miongozi mwa walioshiriki mdahalo huo, ambapo masuala mbalimbali yalijadiliwa, yakiwa ni pamoja na vita vya Russia nchini Ukraine, uhamiaji, uchumi, dawa za kulevya na hata kujibu swali kuhusu iwapo wankiwa ris watamsamehe rais wa zamani Trump, anayekabiliwa na kesi kadhaa mahakamani.

Kufikia Jumatano, wachache wa walioshiriki mdahalo huo walisikika kumkosoa Trump, ispokuwa aliyekuwa Gavana wa New Jersey Chris Christie.

Vivek Ramaswamy.
Vivek Ramaswamy.

Wengine, kama vile Gavana wa Florida, Ron DeSantis, ambaye anamfuata Trump kwa mbali katika utafiti wa maoni na Gavana wa zamani wa South Carolina, Nikki Haley, wamechukua msimamo wa wastani katika kumkosoa Trump, wakitarajia kushawishi wanachama ambao ni waaminifu kwake, kwamba wanaweza kutekeleza agenda yake ya zamani ya "Make America Great Again" bila vikwazo vya kisheria na utata mwingine, unaomkumba Trump.

"Ni lazima tumg'oe Joe Biden na sera yake ya uchumi," alisema Desantis, ambaye pia alisema kuna umuhimu wa kulinda mpaka wa kusini wa Marekani "ambao unadhibitiwa na wahalifu."

Vivek Ramaswamy, 38, alijibizana vikali na wawaniaji wengine, pamoja na Chris Christie, kuhusu masuala kadhaa.

Mwanasiasa huyo mwenye umri mdogo zaidi kati ya wawaniaji wote waliokuwemo, na ambaye anafahamika kama mwenye misimamo tata, alisema iwapo atachaguliwa rais, hataunga mkono Marekani kwendelea kutoa usaidizi wa kivita kwa Ukraine katika vita vyake na Russia, akiongeza kwamba fedha zinzotumika Ukraine zinafaa kwelekezwa "kwingineko ambako zinahitajika zaidi."

Haley alimkosa na kusema kwamba ananuia kuikabidhi Ukraine kwa mikono ya Russia.

"Hana tajriba yoyote ya mahusiano ya kimataifa," aliongeza.

"Nadhani tunahitaji mtu wa kizazi tofauti kuongoza nchi hii," alisema, akimtazama Pence ambaye alikuwa amesema kwamba Marekani haihitaji mtu asiye na ujuzi kuiongoza.

Seneta Tim Scott alisema tangu Rais Joe Biden kuingia madarakani, mamilioni ya watu wamevuka mpaka kinyume cha sheria na kuingia Marekani.

Awali kwenye mdahalo huo, wengi walkubaliana na jinsi Pence alivyoshughulikia suala la uvamizi wa majengo ya bunge tarehe 6, Januari mwaka 2021.

Trump, ambaye anakabiliwa na kesi kadhaa, aliamua kushiriki mahojiano kwenye mtandao wa X/Twitter na Tucker Carson, mtangazaji wa zamani wa shirika la FOX News, ambayo yalikuwa yamerekodiwa.

Forum

XS
SM
MD
LG