Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:57

Kesi dhidi ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kuanza kusikilizwa Machi mwakani


Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump.
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump.

Kesi dhidi ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kutokana na madai ya kujaribu kuingilia matokeo ya uchaguzi wa rais wa 2020 itaanza kusikilizwa Machi mwaka ujao, jaji mmoja wa serikali amesema Jumatatu.

Jaji Tanya Chutkan ambaye atasikiliza kesi hiyo amesema itaanza Machi 4 siku moja kabla ya Super Tuesday, siku ambayo majimbo 15 hupiga kura za kuteua wagombea wa urais kwenye uchaguzi mkuu. Takwimu zinaonyesha kwamba kufikia sasa Trump anaongoza miongoni mwa watu wanaonuia kuwania urais kupitia chama cha Repablikan.

Waendesha mashitaka walikuwa wamependekeza kesi hiyo ianze Januari 2 mwakani, wakati mawakili wa Trump wakiomba isogezwe hadi Aprili 2026, miaka miwili baada ya uchaguzi wa mwaka ujao kufanyika. Jaji Chutkan hata hivyo alikataa mapendekezo hayo, wakati tarehe aliyotaja ikionekana kuathiri kampeni ya Trump, pamoja na kesi nyingi zinazomkabili.

Forum

XS
SM
MD
LG