Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 00:27

Uchaguzi 2024: Uwezekano wa kuchaguliwa tena Rais wa zamani Donald Trump unahojiwa


(FILES) Former US President Donald Trump speaks at the Conservative Political Action Conference 2022 (CPAC) in Orlando, Florida, on February 26, 2022.
(FILES) Former US President Donald Trump speaks at the Conservative Political Action Conference 2022 (CPAC) in Orlando, Florida, on February 26, 2022.

Katika kinyang’anyiro cha urais mwaka 2024, uwezo wa kuchaguliwa tena Rais wa zamani Donald Trump unahojiwa baada ya kujisalimisha huko Georgia katika kesi ya wiki iliyopita inayohusu ubadhirifu katika uchaguzi.

Ukusanyaji maoni wa taifa bado unaonyesha kuwa Trump anaongoza mbele ya warepublican wenzake watarajiwa kwa idadi kubwa.

Siku kadhaa baada ya jela ya Atlanta kumuandikisha rais wa zamani Donald Trump na hilo kuwa habari kubwa kote duniani, utashi wake wa kisiasa kwa mara nyingine tena unafuatiliwa kwa karibu.

Trump hivi sasa anakabiliwa na makosa 91 ya uhalifu kutokana mashtaka manne.

Miognoni mwa wagombea watarajiwa wanaowania uteuzi wa Republican kugombea urais, Gavana wa zamani wa New Jersey Chris Christie, ambaye alihojiwa na kituo cha televisheni cha ABC katika kipindi cha This Week, alipendekeza kwamba Trump ni mzigo kwa chama chake.

“Washindani wangu wakubwa wanaamini kuwa unaweza kushtakiwa kwa uhalifu kama mteuli wa urais na halafu wanakuunga mkono na kwamba unweza kushinda. Nadhani hilo haliwezekani,” anasema Christie.

Mgombea urais wa Republican Vivek Ramaswamy, ambaye, pamoja na Christie, walishiriki wiki iliyopita katika mdahalo wao wa kwanza, alikiri mafanikio ya Trump alipohojiwa na kituo cha Televisheni cha NBC katika kipindi cha Meet the Press.

Ramaswamy anasema “nataka kujenga msingi ambao Trump aliuweka. Kwa kweli, nitamkaribisha kama mshauri. Sitaki kujifunza tena mambo hay ohayo. Nataka kuanzia pale alipoachia yeye.”

Matatizo ya kisheria ya Trump hayatakuwa sehemu ya mkakati wa kampeni ya Rais Joe Biden kutaka kuchaguliwa tena mwaka 2024, mwenyekiti mwenza wa kampeni ya Biden, Cedric Richmond amekiambia kituo cha televisheni cha ABC.

“Lakini nitasema nini Rais Biden na Makamu Rais Harrisn ni kwamba siku zote wamewalenga watu wa Marekani. Kwahiyo wataendelea kufanya kazi yao katika kushusha gharama, kuongeza mishahara, kujenga tena watu wa daraja la kati,” anasema Richmond.

Lakini wakati umri wa Biden ukiendelea kuwapa wasi wasi wapiga kura wademocrat, Seneta Huru Bernie Sanders, ambaye alionekana kwenye kituo cha televisheni cha NBC, alipendekeza kugeuza mtizamo na kulenga kile ambacho ni muhimu katika masuala ya sera.

Bernie Sanders anasema “unaamini kwamba wanawake wana haki ya kudhibiti miili yao? Ndiyo, rais amekuwa na msimamo thabiti kwa hilo. Unadhani kwamba mabadiliko ya hali ya hewa ni kweli? Au unakubaliana na warepublican kwamba hilo si suala zito?”

Wakati huo huo, Trump, ambaye amekanusha kufanya makosa yoyote, anatumia uchunguzi wake wa kihalifu unaofanywa ili kusukuma mbele ajenda yake kuwania urais mwaka 2024.

Hiyo inajumuisha kuhamasisha picha aliyopigwa wakati alipojisalimisha jela ichapishwe katika kila aina ya vifaa kwa ajili ya malengo ya uchangishaji fedha.

Forum

XS
SM
MD
LG