Wakati wa ziara yake rasmi , rais Biden aliahidi msaada mwingine wa dola milioni 600 jumatano kwa mradi mkubwa wa reli wa nchi kadhaa barani Afrika kama moja ya sera ya mwisho ya mambo ya nje chini ya utawala wake. Aliwaambia viongozi wa Afrika kwamba bara lenye rasilimali nyingi na zaidi ya watu bilioni 1.4 limeachwa nyuma kwa muda mrefu.
Biden alitumia siku yake ya mwisho kuitembelea Angola katika ziara iliyosubiriwa kwa muda mrefu katika nchi zilizo chini ya jangwa la sahara, kama rais na Kwenda hadi mji wa mwambao wa LOBITO na kutembelea kituo cha bandari cha Atlantiki ambacho ni sehemu ya uundaji upya wa reli ya Lobito Corridor.
Hata hivyo Biden ameelezea kama uwekezaji mkubwa katika mradi wa reli nje ya Marekani.
Forum