Katika ziara hiyo leo Jumatano Rais Biden ameutembelea mji wa Lobito, uliopo pwani ya magharibi mwa Afrika katika siku ya mwisho ya ziara yake nchini Angola.
Biden aliandamana na mwenyeji wake Rais João Lourenço, Rais wa Zambia Hakainde Hichilema, wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi na Makamu Rais wa Tanzania Philip Mpango.
Biden ametumia siku ya tatu na ya mwisho ya ziara yake nchini Angola kuangazia mradi wa ujenzi wa reli ya Lobito, ambapo Marekani na washirika wake wakuu wanafadhili ujenzi wa reli yenye urefu wa kilomita 13,000 kutoka Zambia hadi Angola kupitia Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Viongozi hao vile vile wamekutana na wawakilishi wa makampuni yatakayofaidika na mradi huo ikiwemo ya mawasiliano inayoimarisha huduma zake katika eneo hilo, kampuni ya uzalishaji chakula na kampuni ya Pennyslvania inayotengeneza vyuma za kujenga madaraja, yenye mkataba wa kuwasilisha vifaa vyake nchini Angola.
Forum