Miongoni mwa walioachiliwa kuna idadi ndogo sana kati ya mamia ya wafungwa wa kisiasa walioko jela kwa kuupinga utawala wa kijeshi tangu jeshi liliponyakua madaraka mwezi Februari mwaka 2021 kutoka kwa serikali iliyochaguliwa ya Aung San Suu Kyi.
Kunyakua huko madaraka kimabavu kulikabiliwa na upinzani mkubwa kwa njia ya amani, ambao tangu wakati huo umegeuka mapambano ya silaha yaliyosambaa nchi nzima.
Hakuna ishara yoyote kwamba Aung San Suu Kyi ambaye ameshikiliwa kiholela na jeshi tangu liliponyakua madaraka, atakuwa miongoni mwa wafungwa walioachiliwa.
Suu Kyi mwenye umri wa miaka 79, anatumikia kifungo cha miaka 27 baada ya kukutwa na hatia katika msururu wa mashtaka ya kisiasa yaliyowasilishwa na jeshi.
Forum