Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 04, 2025 Local time: 18:42

Dereva wa gari aua watu 10 New Orleans katika shambulio linalochunguzwa kama la kigaidi


Wachunguzi wa FBI wafika kwenye eneo la tukio la shambulio la dereva aliyeua watu 10 New Orleans, Jan 1, 2025. Picha ya AFP
Wachunguzi wa FBI wafika kwenye eneo la tukio la shambulio la dereva aliyeua watu 10 New Orleans, Jan 1, 2025. Picha ya AFP

Watu kumi waliuawa na 35 kujeruhiwa baada ya mshukiwa kuvurumisha gari lake kwenye umati wa watembea kwa miguu katika Barabara yenye shughuli nyingi ya French Quarter huko New Orleans leo saa tisa na robo alfajiri siku ya Jumatano kwenye mtaa wa Bourbon.

Eneo hilo ambalo linajulikana sana duniani kote kama moja ya maeneo makubwa ya karamu za mkesha wa mwaka mpya, kulikuwa na umati wa watu wakijiandaa kwa ajili ya mchezo wa mchujo wa Sugar Bowl kati ya timu za vyuo vikuu ambao utafanyika jioni hii.

Mshukiwa aliuawa baada ya mapambano na polisi, maafisa wa polisi wameliambia shirika la Habari la AP.

Maafisa hawakutoa maelezo ya uchunguzi hadharani na walizungumza na AP katika misingi ya kutotajwa majina.

“Alikuwa na nia mbaya ya kutekeleza mauaji na kufanya uharibifu,” Kamishna wa polisi Anne Kirkpatrick alisema.

Alisema maafisa wa polisi watafanya kazi kuhakikisha usalama unaimarishwa wakati wa mchezo huo wa Sugar Bowl, na kubaini kwamba mchezo utafanyika kama ulivyopangwa.

Forum

XS
SM
MD
LG