Carl Skau, naibu mkurugenzi mtendaji wa Mpango wa Chakula Duniani, alisema WFP iliweza tu kufikisha misaada kwa Wapalestina 300,000 hadi 400,000 mwezi Novemba katika Ukanda wa Gaza kutokana na mashambulizi ya kijeshi ya Israel yanayoendelea na uporaji unaofanyika kwa misafara.
Kiwango cha chakula kilichoruhusiwa na Israel kimepungua katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, ikichangiwa na uamuzi wa Jumapili wa Umoja wa Mataifa wa kusitisha upelekaji misaada kutoka kwenye kivuko kikuu kuelekea eneo hilo kwa sababu ya tishio la magenge yenye silaha kupora misafara.
Wataalamu tayari wameonya kuhusu baa la njaa katika eneo la kaskazini mwa Gaza, ambalo wanajeshi wa Israel wamekaribia kulitenga kabisa tangu mapema Oktoba, wakisema wanapambana na wapiganaji wa Hamas waliojipanga upya huko.
Uvamizi wa Israeli huko Gaza, ulichochewa na shambulio la Hamas Oktoba 7, 2023 kusini mwa Israeli, ambalo limesababisha karibu wakazi wote wa eneo hilo kukimbia makazi yao.
Forum