Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 06:07

HRW laishutumu Israel kutenda uhalifu wa kivita huko Gaza


Picha za watu waliotekwa nyara wakati wa shambulizi la Hamas la Oktoba 7, 2023.
Picha za watu waliotekwa nyara wakati wa shambulizi la Hamas la Oktoba 7, 2023.

Kundi la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch Alhamisi limeishutumu Israel kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu kutokana na vita vyake dhidi ya kundi la Hamas huko Gaza, dai ambalo imelikanusha.

Ripoti ya kundi hilo imesema kuwa Israel imewakosesha watu makazi, na kuwalazimisha kuhama, kwa hivyo imetekeleza uhalifu wa kuhamisha watu kwa lazima, wakati matendo yake pia yakifanana na chuki dhidi ya kundi moja, kwa kuwa kuna maeneo ambayo Wapalestina hataweza kurudi tena.

Human Rights Watch imesema kuwa uhamishaji wa watu umeenea kote, kuna ushahidi kuwa unafanyika kulingana na sera ya serikali. Katika majibu yake, Israel imeikashifu ripoti hiyo ikisema kuwa kundi hilo linatumia madai yasiyo na msingi , yenye uongo na yaliyo mbali na ukweli.

Wizara ya mambo ya nje ya Israel imesema kuwa juhudi za Israel zinalenga kuliangamiza kundi la Hamas na wala siyo wakazi wa Gaza, kinyume na Hamas ambalo hutumia binadamu kama ngao pamoja na kuweka miundo mbinu ya kigaidi kwenye maeneo ya makazi.

Msemaji wa wizara hiyo Oren Marmorstein katika taarifa yake amesema kuwa Israel itaendelea kufanya operesheni zake kulingana na misingi ya kanuni za vita.

Forum

XS
SM
MD
LG