Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 03:17

Ujerumani ilipokea tahadhari kuhusu mshukiwa wa shambulizi kwenye soko la Christmas


Watu wengi wajitokeza kuweka maua na mishuma kwenye eneo la shambulizi la gari kwenye soko la Christmas, Disemba 22, 2024. Picha ya Reuters
Watu wengi wajitokeza kuweka maua na mishuma kwenye eneo la shambulizi la gari kwenye soko la Christmas, Disemba 22, 2024. Picha ya Reuters

Mamlaka za Ujerumani zilipokea taarifa za tahadhari mwaka jana kuhusu mshukiwa wa shambulizi la gari kwenye soko la Christmas, ofisi ya serikali imesema Jumapili, huku maelezo zaidi yakitolewa kuhusu watu watano waliouawa katika shambulizi hilo.

“Tulipokea tahadhari hiyo kwa uzito, kama tunavyochukulia vidokezo vingine vingi,” ofisi ya uhamiaji na wakimbizi ilisema Jumapili kwenye mtandao wa X kuhusu kidokezo ambacho ilisema ilipokea mwishoni mwa msimu wa joto mwaka jana.

Lakini ofisi hiyo pia imebaini kwamba sio mamlaka ya kufanya uchunguzi na ilitoa taarifa hizo kwa mamlaka husika, kulingana na utaratibu katika kesi kama hizo.

Haikutoa maelezo zaidi kuhusu mshukiwa au aina ya tahadhari.

Polisi katika mji wa Magdeburg, ambako shambulizi lilifanyika Ijumaa jioni, wamesema Jumapili kwamba waliouawa ni wanawake wanne wenye umri ulio kati ya miaka 45, 52, 67 na 75, pamoja na mtoto wa kiume wa miaka 9.

Maafisa walisema watu 200 walijeruhiwa, na 41 miongoni mwao walijeruhiwa vibaya.

Mamlaka zilimtaja mshukiwa kama daktari raia wa Saudi Arabia ambaye aliwasili Ujerumani mwaka 2006 na alikuwa mkazi wa kudumu.

Jumamosi jioni, mshukiwa alifikishwa mbele ya jaji, katika kesi iliyosikilizwa kwa faragha, aliamuru mshukiwa aendelee kukaa ndani kwa kusubiri mashitaka.

Forum

XS
SM
MD
LG