Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:19

Guterres azungumzia athari za mabadilko ya hali hewa akiwa ziarani Lesotho


Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, Alhamisi ameziomba nchi tajiri kutimiza ahadi zao ya kuzisaidia nchi masikini katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Hayo ameyasema wakati alipokuwa akitoa hotuba yake kwenye bunge la Lesotho, huku akisistiza kuwa ana matumaini kwamba hivi karibuni Afrika itapata viti vya kudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Guterres yupo kwenye ziara ya siku tatu kusini mwa Afrika, na Jumatano aliitembelea Afrika Kusini. Wakati akiwa Lesotho nchi isiyo na bandari na inayopakana na Afrika Kusini, alitembelea bwawa la Katse ambalo ni sehemu ya mpango wa serikali wa kuimarisha hifadhi ya maji.

Suala kuu ambalo Guterres ameangazia wakati wa ziara yake ni kuhusu fedha zinazohitajika kwa nchi masikini barani Afrika na kwingineko katika kukabiliana na ongezeko la joto duniani. Ingawa Afrika inachangia asilimia ndogo sana ya ongezeko la joto, ndilo bara lililoathirika zaidi.

Mwezi uliopita mataifa yalikubaliana kwenye mkutano wa Azerbaijan kuchanga takriban dola milioni 300 kwa mwaka ili kuzisaidia nchi masikini kukabiliana na ongezeko la joto duniani. Fedha hizo hata hivyo ni kiasi kidogo zikilinganishwa na dola trilioni 1 ambazo mataifa yanayoendelea yalikuwa yanaitisha ili kukabiliana na janga hilo.

Guterres pia alisema kuwa mfuko mpya uliobuniwa kukadiria hasara na uharibifu kutokana na majanga ya asili yaliyosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa kwenye nchi masikini, ni lazima uanze kufanya kazi na kuchangiwa ipasavyo na wale wanaohusika kwenye uharibifu wa mazingira.

Forum

XS
SM
MD
LG