Katika taarifa yake, Umoja wa Mataifa ulisema “uamuzi usio wa kawaida” wa kusitisha shughuli na program zote katika mkoa wa kaskazini wa Saada ulisababishwa na ukosefu wa mazingira ya usalama yanayohitajika na uhakika wa usalama.
Waasi katika miezi ya hivi karibuni waliwashikilia wafanyakazi kadhaa wa Umoja wa Mataifa, pamoja na watu wanaoshirikiana na makundi ya misaada, mashirika ya kiraia na Ubalozi wa zamani wa Marekani katika mji mkuu wa Yemen, Sanaa. Hakuna mfanyakazi hata mmoja wa Umoja wa Mataifa aliyeachiliwa.
Taarifa ya Umoja wa Mataifa imesema hatua hiyo ya kusitisha kwa muda shughuli inakusudia kuwapa Wahouthi na taasisi hiyo ya kimataifa muda wa “kuafikiana juu ya kuachiliwa kwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa walioshikiliwa kiholela na kuhakikisha msaada muhimu wa kibinadamu unaohitajika” unaotolewa katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi.
Forum