Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 03, 2025 Local time: 04:19

Hamas yabadili msimamo wake na kusema itawaachilia mateka zaidi wa Israel


Mateka watatu wanawake wa Israel walioachiliwa na Hamas, Januari 19, 2025.
Mateka watatu wanawake wa Israel walioachiliwa na Hamas, Januari 19, 2025.

Hamas Alhamisi ilisema itawaachilia mateka watatu zaidi wa Israel mwishoni mwa juma kama ilivyopangwa kwa kubadilishana na wafungwa wa Kipalestina.

Hatua hiyo imeongeza matarajio ya kusuluhisha mzozo mkubwa kuhusu sitisho la mapigano katika Ukanda wa Gaza.

Israel, ikiungwa mkono na Rais wa Marekani Donald Trump, ilisema itaanza tena mapigano iwapo mateka hao hawataachiliwa, lakini haikutoa maelezo kuhusu taarifa hiyo ya Hamas.

Hamas ilikuwa imetishia kuchelewesha mpango wa kuwaachilia mateka kwa sababu Israel haitekelezi ahadi zake katika makubaliano ya kusitisha mapigano.

Israel hairuhusu makazi ya kutosha, vifaa vya matibabu, mafuta na tingatinga za kusafisha vifusi hadi Gaza, kati ya madai mengine ya ukiukaji wa sitisho la mapigano.

Pande zote mbili zimebadilishana mateka mara tano tangu sitisho la mapigano lilipoanza kutekelezwa Januari 19, mateka 21 wa Israel na zaidi ya wafungwa 730 wa Kipalestina wakiwa wameachiliwa kufikia sasa katika awamu ya kwanza ya makubaliano ya sitisho la mapigano.

Forum

XS
SM
MD
LG