Katika uchaguzi wa kwanza wa bunge nchini Chad katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja , chama tawala Patriotic Salvation Movement kilipata viti 124 kati ya 188, huku idadi ya wapiga kura ikiwa asilimia 51.5, kulingana na matokeo ya awali yaliyotangazwa Jumamosi jioni na Ahmed Bartchiret, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi.
Uchaguzi wa bunge, pamoja na uchaguzi wa serikali za mitaa na mikoa, ni muendelezo wa kipindi cha mpito kuelekea utawala wa kidemokrasia baada ya Mahamat Idriss Deby kuchukua madaraka kama mwanajeshi mwaka 2021.
Aliingia madarakani baada ya kifo cha baba yake na rais wa muda mrefu Idriss Deby Itno, ambaye aliongoza kwa miongo mitatu. Deby alishinda uchaguzi wa rais wenye utata wa mwaka jana.
Forum