Ni mkasa wa hivi karibuni uliohusisha watu wanaotaka kufika Ulaya kupitia nchi hiyo ya Afrika Kaskazini inayokumbwa na machafuko.
Kaburi la kwanza la watu wengi likiwa na miili 19 liligunduliwa siku ya Ijumaa katika shamba katika mji wa kusini mashariki wa Kufra, idara ya usalama ilisema, na kuongeza kuwa maafisa walichukuwa miili hiyo kwa ajili ya vipimo vya uchunguzi wa maiti.
Maafisa waliweka picha kwenye ukurasa wa Facebook zikionyesha maafisa wa polisi na madaktari wakichimba mchangani na kuopoa maiti zilizokuwa zimefungwa kwenye blanketi.
Shirika moja la hisani The al-Abreen charity, ambalo linasaidia wahamiaji mashariki na kusini mwa Libya, lilisema kuwa baadhi ya watu hao walipigwa risasi na kuuawa kabla ya kuzikwa.
Kaburi tofauti la watu wengi, lenye takriban miili 30, pia liligunduliwa Kufra baada ya uvamizi wa kituo cha usafirishaji haramu wa binadamu, kulingana na Mohamed al-Fadeil, kiongozi wa idara ya usalama huko Kufra.
Manusura walisema karibu watu 70 walizikwa kwenye kaburi hilo, aliongeza.
Forum