Ndege iliyokuwa inambeba Duterte iliondoka Manila Jumanne jioni. Alikamatwa baada ya kuwasili na familia yake kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Manila Jumanne asubuhi akitokea Hong Kong, chini ya hati ya kumkamata ya ICC.
Mahakama hiyo ya kimataifa iliamuru akamatwe baada ya kumshtumu kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu kutokana na sera yake mbaya ya kutokomeza biashara ya dawa za kulevya ambayo alikuwa anaisimamia akiwa madarakani, serikali ya Ufilipino imesema.
ICC imekuwa ikifanya uchunguzi wa mauaji makubwa kuhusiana na sera hiyo ya Duterte alipokuwa akihudumu kama meya wa mji wa kusini mwa Ufilipino wa Davao na baadaye kuhudumu kama rais.
Forum