Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 31, 2025 Local time: 06:16

Israel yakata huduma ya umeme kwa Gaza


Mji wa Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza
Mji wa Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza

Israel Jumapili ilitangaza kwamba imekata huduma ya umeme kwa Gaza. Matokeo ya hatua hiyo hayakueleweka haraka, lakini eneo la Gaza linapata umeme kutoka Israel ili kuzalisha maji ya kunywa.

Hamas imeitaja hatua hiyo kama sehemu ya “sera ya Israel ya kusababisha njaa.”

Wiki iliyopita, Israel ilifunga usafirishaji wa bidhaa kwa Wapalestina zaidi ya milioni 2, ikikumbusha hatua kali ilizochukua siku za mwanzo za vita vyake dhidi ya Hamas.

Inaishinikiza Hamas kukubali kuongeza muda wa utekelezaji wa sitisho la mapiganio katika awamu ya kwanza. Awamu hiyo ilimalizika mwishoni mwa juma lililopita.

Israel inataka Hamas iwaachilie nusu ya mateka wanaobaki ili kufanikisha mazungumzo ya sitisho la mapigano la kudumu.

Hamas badala yake inataka kuanza mazungumzo juu ya awamu ya pili ngumu sana ya kusitisha mapigano, ambayo ingepelekea kuachiliwa kwa mateka wanaosalia huko Gaza, kuondolewa kwa wanajeshi wa Israel na amani ya kudumu.

Inaaminika kuwa Hamas bado inashikilia mateka 24 walio hai na miili ya watu wengine 35.

Forum

XS
SM
MD
LG