Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 25, 2025 Local time: 13:18

Rais wa serikali ya mpito Syria ahudhuria kikao cha kujadili mustakabali wa Gaza


FILE - Syria's de facto leader Ahmad al-Sharaa walks in the presidential palace ahead of a meeting, in Damascus, Dec. 28, 2024.
FILE - Syria's de facto leader Ahmad al-Sharaa walks in the presidential palace ahead of a meeting, in Damascus, Dec. 28, 2024.

Rais wa serikali ya mpito ya Syria Ahmad al-Sharaa amewasili Cairo kuhudhuria  mkutano wa viongozi wa nchi za Kiarabu.

Viongozi hao wanatarajiwa kuidhinisha mapendekezo ya Misri yanayokinzana na ya Rais wa Marekani Donald Trump ya kutaka watu kuondolewa ukanda wa Gaza na kuigeuza sehemu hiyo kuwa mandhari ya Mashariki ya Kati.

Huu ni mkutano wa kikanda unaohudhuriwa na Al-Sharaa tangu alipoingia madarakani.

Uongozi mpya wa Syria, ukiongozwa na kundi la Kiislamu la Hayat Tahrir al-sham, uliupindua utawala wa familia ya Assad mwezi Desemba, baada ya kutawala Syria kwa zaidi ya miaka 50.

Mkutano huo wa leo Jumanne, umeandaliwa na Rais wa Misri Abdel-Fattah el-Sissi, na umewaleta pamoja viongozi wa Saudi Arabia, na Umoja wa Falme za Kiarabu ambao msaada wao unachukuliwa kuwa muhimu kwa mpango wa baada ya vita.

Trump alilishitua eneo hilo mwezi uliopita alipopendekeza kwamba karibu wakazi wa Gaza milioni 2 waondoke Gaza na kwenda nchi nyingine na kwamba Marekani itachukua umiliki wa Gaza ambao umeharibiwa kutokana na vita, na kuigeuza sehemu hiyo kuwa mandhari ya Mashariki ya Kati.

Misri imeandaa mpango mbadala ambapo Wapalestina watawekwa katika sehemu salama ndani ya Gaza wakati ujenzi mpya unapoendelea, na kundi la Hamas litapokeza uongozi wa Gaza kwa utawala mbadala wa wanasiasa wasiokuwa na mirengo hadi mamlaka ya Palestina itakapochukua uongozi.


Forum

XS
SM
MD
LG