Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Machi 30, 2025 Local time: 23:07

Usitishaji wa kudumu wa mapigano Gaza bado haujafikiwa


Awamu ya kwanza ya mapatano ya Israel na Hamas inamalizika Jumamosi, na mazungumzo juu ya hatua inayofuata ya kupata usitishaji wa kudumu wa mapigano, hadi sasa hayajakamilika.

Usitishaji huo wa mapigano ulianza Januari 19 baada ya vita vya zaidi ya miezi 15 vilivyosababishwa na shambulio la kigaidi la Oktoba 7, 2023 dhidi ya Israel na kundi la Hamas, ambalo ni baya zaidi kuwahi kutokea katika historia ya nchi hiyo.

Kwa muda wa wiki kadhaa, Hamas iliwaachia huru mateka 25 walio hai na kurejesha miili ya wengine wanane kwa Israel, kwa kubadilishana na mamia ya wafungwa wa Kipalestina waliokuwa wakishikiliwa katika jela za Israel.

Awamu ya pili ya mapatano tete, ambayo yalisimamiwa na Marekani, Qatar na Misri baada ya miezi kadhaa ya mazungumzo magumu, inapaswa kuanza Jumapili, na kuhakikisha kuachiliwa kwa dazeni ya mateka ambao bado wako Gaza.

Forum

XS
SM
MD
LG