Huu ni Mkutano wa kwanza wa mawaziri wa mambo ya nje kutoka kundi la G20 yenye Uchumi mkubwa tangu Afrika kusini ilipochukua nafasi ya urais Desemba mwaka jana.
Uhusiano wa kidiplomasia baina ya Pretoria na Washington chini ya utawala mpya wa rais Donald Trump umekuwa na Dosari.
Trump amekata misaada katika serikali inayoongozwa na watu Weusi ya Afrika Kusini kufuatia amri yake ya kiutendaji wiki iliyopita.
Katika agizo hilo Trump alisema waafrika kusini ambao ni walowezi wa kikoloni wa uholanzi walikuwa wanalengwa na sheria mpya inayoruhusu serikali kunyakua ardhi binafsi.
Forum