Salamu za rambirambi zilizidi kumiminika kwa “baba mwanzilishi wa nchi hiyo ya kusini mwa Afrika, huku Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akimpongeza Nujoma kama mfano kwa mapambano ya nchi yake dhidi ya utawala wa wazungu walio wachache.
Kiongozi wa kundi la ukombozi la SWAPO alifariki Jumamosi jioni baada ya kulazwa hospitali kwa wiki tatu, akipambana na ugonjwa ambao “hakuweza kuupona”, Rais wa Namibia Nangolo Mbumba alisema katika taarifa.
“Kwa huzuni na maskitiko makubwa” Mbumba alisema akitangaza “kufariki kwa mpigania uhuru wetu anayeheshimika na kiongozi wetu wa mapinduzi”.
“Baba yetu Mwanzilishi aliishi maisha marefu na yenye matokeo muhimu ambapo alitumikia kwa njia ya kipekee wananchi wa nchi yake anayoipenda,” aliongeza.
Namibia ilipata uhuru mwaka 1990, huku Nujoma akishinda uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia mwaka huo. Utasikia mengi zaidi katika ripoti zetu baadaye kidogo.
Forum