“Tuna wasiwasi na kile kinachoonekana kuwa kampeni ya upotoshaji na propaganda inayolenga kupotoshwa kwa taifa letu,” serikali imesema.
Imeongeza kusema kwamba inasikitisha kuona matamshi hayo yanaonekana kupata upendeleo miongoni mwa watoa maamuzi wa Marekani.
Rais Trump alisema sheria hiyo itaiwezesha serikali ya Afrika Kusini kunyakua mali za kilimo za Waafrikana walio wachache bila fidia.
Amri ya kiutendaji, pia ilibainisha migongano ya sera za kigeni kwa nchi hizo mbili kuhusu vita vya Gaza.
Afrika Kusini imesema imezingatia amri ya utendaji ya Trump, lakini ikaongeza, ina na msingi wake kuwa kuna si sahihi na hauna ukweli.
Forum