Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 02, 2025 Local time: 18:07

Wazungu wa Afrika Kusini wamuunga mkono Trump


Baadhi ya Wazungu wa Afrika Kusini, Jumamosi walionyesha kumuunga mkono Rais Donald Trump, kwa kukusanyika katika Ubalozi wa Marekani mjini Pretoria kudai wao ni waathirika wa ubaguzi wa rangi na serikali yao wenyewe.

Mamia ya waandamanaji walishika mabango yaliyoandikwa “Asante Mungu kwa ajili ya Rais Trump” na kuonyesha ujumbe mwingine wa kukosoa kile wanachokiona kuwa sheria za kibaguzi zilizoanzishwa na serikali ya Afrika Kusini zinazowabagua wazungu walio wachache.

Wengi wanatoka jumuiya ya Afrikana ambayo Trump alizingatia katika amri ya utendaji wiki moja iliyopita ambapo alipunguza misaada na usaidizi kwa serikali ya Afrika Kusini inayoongozwa na Weusi.

Katika agizo hilo, Rais Trump amesema Waafrika Kusini, ambao ni walowezi wa kikoloni wa Uholanzi, wanalengwa na sheria mpya inayoruhusu serikali kuchukua ardhi binafsi.

Afrika Kusini imekanusha madai ya Rais Trump.

Forum

XS
SM
MD
LG