Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 27, 2025 Local time: 19:49

Trump aiwekea ushuru Colombia baada ya nchi hiyo kukataa kupokea wahamiaji waliofukuzwa Marekani


Rais Donald Trump na Rais wa Colombia Gustavo Petro
Rais Donald Trump na Rais wa Colombia Gustavo Petro

Rais wa Marekani Donald Trump Jumapili alisema kwamba ameamuru ushuru, marufuku ya viza na hatua nyingine za ulipizaji kisasi zichukuliwe dhidi ya Colombia baada ya serikali ya nchi hiyo kuzikatilia ndege mbili zilizokuwa zinabeba wahamiaji kuingia nchini humo.

Trump alisema hatua hizo ni muhimu, kwa sababu uamuzi wa Rais wa Colombia Gustavo Petro “unahatarisha” usalama wa taifa wa Marekani.

“Hatua hizi ni mwanzo tu,” Trump aliandika kwenye mtandao wake wa Kijamii Truth Social.

“Hatutairuhusu serikali ya Colombia kukiuka majukumu yake ya kisheria inapohusu kukubali kuwarejesha wahalifu waliowalazimisha kuingia Marekani.”

Mapema Jumapili, Petro alisema kwamba serikali yake haitokubali ndege zinazobeba wahamiaji waliofukuzwa kutoka Marekani kuingia nchini mwake hadi pale utawala wa Trump utakapoweka mkataba ambao unawapa “heshima”.

Petro alitoa taarifa kupitia mtandao wa X, na ujumbe mmoja ulijumuisha video mpya ya wahamiaji wanaoripotiwa kupelekwa Brazil baada ya kufukuzwa wakiwa kwenye uwanja wa ndege wakifungwa kamba kwenye mikono na miguu yao.

“Mhamiaji sio mhalifu na lazima apewe heshima ambayo binadamu anastahili,” Petro alisema.

Forum

XS
SM
MD
LG