Ametangaza kumuunga mkono Makamu Rais Kamala Harris.
Rais Joe Biden jana Jumapili ametangaza anajiondoa ktika ushindani wa kuwania tena urais mwaka huu wa 2024.
Takriban wajumbe wote 3,896 katika mkutano mkuu wa Kitaifa wa Democratic unaofanyika huko Chicago mwezi ujao wameahidi kumpa kura Biden, ambaye alishinda kila uchaguzi wa awali kote nchini. Lakini kwa mujibu wa kanuni za DNC, “ahadi” hiyo inaweza kubadilika.
John Fortier, Taasisi ya American Enterprise anaeleza: “Huenda yakawepo baadhi ya mashauriano kama Joe Biden ataamua kujiweka kando, pengine huenda akawashawishi au kuidhinisha au kujaribu kuweka njia kwa Makamu Rais Harris pengine akawa mteuliwa. Lakini hakuna uhakika au nji aya kisheria kwake kubadili na kubadili uungaji mkono wake.”
Wa kwanza katika urithi wa urais, Makamu Rais Kamala Harris atakuwa ndiyo chaguo la kwanza linaloeleweka.
Asilimia 58 ya Wademocrat wanadhani Harris atakuwa rais mzuri, kwa mujibu wa ukusanyaji maoni mpya kutoka AP-NORC. Lakini ni asilimia 30 ya Wamarekani kwa ujumla wanadhani atafanya vizuri. Hadharani, anamuunga mkono Biden.
Kamala Harris, Makamu Rais, Marekani anasema: “Joe Biden ni mteuliwa. Tumemshinda Trump mara moja na tutamshinda tena mara nyingine.”
Kama sehemu ya tiketi ya Biden na Harris, Harris anaweza kutumia fedha za kampeni, ambapo zipo katika kiwango cha dola milioni 91, kwa mujibu wa ripoti yao ya mwisho ya mwezi Juni.
Kumteua Harris, mwanamke mweusi, huenda pia akasaidia kura za Wamarekani Waafrika, kundi muhimu sana katika uungaji mkono wa chama.
Hata hivyo, Wademocrat huenda pia wakata kuepuka kujitokeza kwa suala la kutokuwa na demokrasi katika kutawazwa kwa moja kwa moja, hasa kama wengine wanasema wanataka kuteuliwa.
Wagombea watarajiwa ni pamoja na magavana wa majimbo matatu: Gavin Newsom wa California, Josh Shapiro wa Pennyslvania, na Gretchen Whitmer wa Michigan.
Elaine Kamarck, Taasisi ya Brookings anaeleza kuwa : “Lengo la chama litakuwa kuwa na aina fulani ya mchakato kabla ya mkutano mkuu na katika mkutano mkuu itamruhusu kila anayetaka kuingia katika ushindani kutafuta wajumbe. Inaweza kuwa mambo yoyote yale. Huenda ikawa ni mikutano ya kikanda, inaweza kuwa mdahalo.”
Katika mkutano mkuu, Wademocrat lazima pia waamue ambaye atakuwa makamu rais mteule, na mchakato mwingine huenda ukaleta aina fulani ya hamasa na mgawanyiko.
Jennifer Mercieca, Chuo Kikuu cha Texas A & M anasema: “Yeyote ambaye atakuwa na ukosoaji mkubwa kwa uchaguzi wa Harris huenda ikawa ndiyo kundi fulani katika chama ambalo litapata mgombea mwenza. Lakini unajua, yote ni uvumi tu kwa wakati huu, hatujui kitakachotokea, hatujaona chochote kama hili hapo kabla.”
Kabla ya uchaguzi wa Novemba, hiyo ni misukosuko mingi kwa Wademocrat.
Donald Trump, Mgombea Urais Mteule, Republican anasema: “Sisi haraka sana tutaifanya Marekani iwe nzuri tena.”
Wakati Warepublican wamemaliza tu mkutano wao mkuu, na kuonyesha umoja nyuma ya mgombea wao wa urais, Donald Trump.
Forum