Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 15:50

Biden akataa wito wa kuachia azma yake ya kugombea urais


Rais wa Marekani Joe Biden akiongea na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa maadhimisho ya miaka 75 ya NATO Washington, Julai 11, 2024.
Rais wa Marekani Joe Biden akiongea na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa maadhimisho ya miaka 75 ya NATO Washington, Julai 11, 2024.

Rais wa Marekani Joe Biden amekataa wito wa baadhi ya viongozi wa chama chake cha siasa kuachia azma yake ya kugombea kufuatia mdahalo na Donald Trump mwezi uliopita ambapo Biden mara nyingine alipata shida kujieleza.

Kama Biden siyo mteuliwa wa chama cha Democratic, nani atakuwa mteuliwa? Mwandishi wa VOA Scott Stearns anawaangazia baadhi ya wagombea.

Rais Joe Biden anasema yeye yuko katika kinyang’anyiro ili kushinda.

Rais Joe Biden anasema: “Nadhani mimi ni mtu mwenye sifa za kugombea urais.”

Kufuatia kufanya vibaya katika mdahalo mwishoni mwa mwezi uliopita, baadhi ya viongozi wa chama chake wanamtaka Biden kuachia ngazi kama mgombea mtarajiwa.

Lakini baada ya upigaji wa awali na majimbo, chama cha Democratic hakiwezi kumlazimisha kuondoka, anasema Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Virginia kituo cha siasa Larry Sabato.

Larry Sabato, Chuo Kikuu cha Virginia alieleza: “Kuna njia moja tu kwa mteule kuondolewa, na hiyo ni kwa mteule kuamua kutowania kabla ya mkutano mkuu, kufungua, kuruhusu katika kesi hii, Kamati ya Kitaifa cha Democratic, kuweka kanuni kwa ajili ya mkutano mkuu.”

Kama Biden ataamua kuondoka, makamu rais na mgombea mwenza Kamala Harris atakuwa juu katika orodha ya Democratic kuchukua nafasi yake.

Harris anasema Biden ni mteule wa chama na ameonyesha utiifu wake kwa kumdharau Trump, ambaye ametengana na makamu rais wake wa zamani Mike Pence.

Kamala Harris, Makamu Rais wa Marekani amesema: “Fahamu kati ya Joe Biden na Donald Trump, ni mgombea mmoja tu katika hilo jukwaa ameidhinishwa na makamu wake wa rais – Joe Biden.”

Harris kama mteule wa chama huenda akasaidia kwa upande wa wapiga kura huru, anasema profesa wa sayansi ya siasa wa Chuo Kikuu cha Southern California, Christian Grose.

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris
Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris

Christian Grose, Chuo Kikuu cha Southern California: “Jambo moja kuhusu Kamala Harris ambalo nadhani linamfanya kuonekana kuwa anafaa kuchaguliwa kuliko Biden hivi sasa ni kama ukiangalia ukusanyaji maoni, kuna wapiga kura huru wengi ambao hawajaamua kuhusu yeye hivi sasa ili aweze kuwashawishi watu kwa njia ambayo Biden huenda atashindwa kuwashawishi watu.”

Pia katika orodha isiyo rasmi ya watu ambao huenda wanaweza kuchukua nafasi ya Biden ni Gavana wa California Gavin Newsom.

Yeye pia anasema anamuunga mkono Biden na ameonyesha uungaji mkono wake kwa kumfanyia kampeni rais kuchaguliwa tena huko Michigan hivi karibuni.

Gavin Newsom, Gavana California anasema: “Najali kuhusu matokeo na yeye ameonyesha. Kwahiyo nawaachia wenye mawazo mazuri ya kufanya maamuzi. Lakini siangalii muigizaji, namuangalia amiri jeshi mkuu.”

Gavana wa Michigan Gretchen Whitmer ni miongoni mwa wale ambao wamejadiliwa kuhusu uwezekano wa kuchukua nafasi ya Biden. Yeye pia anasema bado anamuunga mkono rais.

Whitmen alishinda kuchaguliwa tena katika jimbo muhimu ambalo linaweza kuelemea upande wowote na ni maarufu kwa wanachama wa Democrat kitaifa kwa kuunga mkono vyama vya wafanyakazi na juhudi za kupambana na ghasia za bunduki.

Gretchen Whitmer, Gavana Michigan anaeleza: “Wiki baada ya wiki hapa Marekani, tunaona vichwa vya habari vibaya ambayo vimezoeleka. Kila sehemu unayoifikiria, au kila hali unaweza kufikiria, imeharibiwa na ghasia za bunduki.”

Gavana wa Kentucky Andy Beshear hajulikani sana kitaifa kuliko Newsom au Whitmer, lakini ni gavana maarufu upande wa kusini ambao umetawaliwa na siasa wa Republican.

Gavana wa Illinois J. B. Pritzker mwenyeji wa mkutano mkuu wa Democratic mwaka huu na ana utajiri binafsi wa kufadhili kiasi kikubwa cha kuwania urais katika dakika za mwisho.

Na pia kuna mke wa rais wa zamani Michelle Obama, ambaye mara kwa mara amekataa dhana yoyote ya kuwania uongozi lakini ambaye ni maarufu kwa wapiga kura wengi. Ukusanyaji maoni uliofanywa na Reuters na Ipsos wiki iliyopita umeonyesha Biden na Trump wako katika nafasi sawa lakini Michelle Obama anamshinda Trump kwa zaidi ya asilimia 10. Sabato anasema hakuna njia itakayomfanya awanie urais.

Michelle Obama
Michelle Obama

Larry Sabato, Chuo Kikuu cha Virginia amesema: “Ni mtu mwerevu sana baada ya miaka minane huko White House kutaka kurejea tena, halafu akawe rais. Kwahiyo, unajua, huenda tukabashiri kuhusu majina ya wote kwa usiku mzima, lakini kinachojalisha ni nani ana utashi mkubwa au uwezo wa kuchangisha fedha na fursa ya kuweka pamoja aina fulani ya muungano ambao huenda ukafanikisha kupata wingi katika mkutano mkuu.”

Kama Biden atabakia katika kinyang’anyiro ubashiri kuhusu majina huenda ukaendelea hadi mwezi ujao wakati wa mkutano mkuu wa chama cha Democratic huko Chicago.

Forum

XS
SM
MD
LG