Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 28, 2024 Local time: 01:24

Marekani na wanachama wengine wa G7 wataipatia Kyiv mkopo wa hadi dola bilioni 50

Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau, Uingereza Rishi Sunak, Rais wa kamisheni ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na rais wa Marekani Joe Biden wakiangalia wanaoruka na miavuli

Marekani  imesema Alhamisi kuwa wao  na wanachama wengine wa G7 wataipatia Kyiv mkopo wa hadi dola bilioni 50 ambao zitalipwa kwa washirika wa Magharibi kwa kutumia mapato ya riba kutoka kwenye  mali za Russia zilizozuiliwa  katika taasisi za kifedha za Magharibi.

Tangazo hilo lilikuja wakati Rais Joe Biden akikutana na viongozi wa Kundi la nchi saba tajiri za demokrasia Alhamisi katika hoteli ya kifahari ya Borgo Egnazia huko Puglia, Italia, katika siku ya kwanza ya mkutano huo.

Biden amekuwa akiwashinikiza viongozi wa G7 kukubaliana na mpango wake kwa washirika wa Magharibi kutoa fedha mapema kwa Ukraine na kulipwa kwa kutumia mapato ya riba kutoka dola bilioni 280 za mali zisizohamishika za Russia.

Forum

XS
SM
MD
LG