Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 19:02

Rais Joe Biden atumia ujumbe wake wa Eid kwa Waislamu kutetea mpango wa kusitisha mapigano Gaza


Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden

Rais Joe Biden alitumia ujumbe wake wa Eid al-Adha kwa Waislamu kutetea mpango wa kusitisha mapigano huko Gaza unaoungwa mkono na Marekani, akisema Jumapili kuwa ndiyo njia bora ya kuwasaidia raia wanaoteseka kutokana” na ukatili wa vita kati ya Hamas na Israel.”

“Raia wengi wasio na hatia wameuawa, wakiwemo maelfu ya watoto. Familia zilikimbia makazi yao na kushuhudia jamii zao zikiharibiwa. Maumivu yao ni makubwa,” Biden alisema katika taarifa.

“Ninaamini sana kwamba pendekezo la awamu tatu la kusitisha mapigano ambalo limewasilishwa na Israel kwa Hamas na kuidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa ni njia bora ya kumaliza ghasia huko Gaza na hatimaye kumaliza vita,” aliongeza.

Marekani imekuwa ikishinikiza Israel na Hamas kukubali rasmi mpango huo wa kusitisha mapigano ulioungwa mkono na wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wiki iliyopita, ambao utaruhusu sitisho la mapigano awamu ya kwanza katiika kipindi cha wiki sita.

Forum

XS
SM
MD
LG