Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:41

Rais wa Marekani Joe Biden ajitoa katika kinyang’anyiro cha kuwania urais.


Rais Joe Biden akiwa na mkewe Jill Biden wakati alipoapishwa na jaji John Roberts kuwa rais wa Marekani Januari 20, 2021. Picha na SAUL LOEB / POOL / AFP
Rais Joe Biden akiwa na mkewe Jill Biden wakati alipoapishwa na jaji John Roberts kuwa rais wa Marekani Januari 20, 2021. Picha na SAUL LOEB / POOL / AFP

Rais Joe Biden amejitoa katika kinyang’anyiro cha urais mwaka 2024 kufuatia mdahalo wake ambao hakufanya vizuri na Rais wa zamani Donald Trump ambaye ni mgombea urais kwa tiketi ya Republican, na kukiingiza chama cha Democratic katika hali ya vurugu miezi michache tu kabla ya uchaguzi mkuu.

Wademocrat wameachwa bila ya mgombea wa wazi, jambo ambalo ni la kushangaza kwa uchaguzi ambao wengi katika chama wanadai ni kati ya matokeo muhimu sana katika maisha kwasababu ya mipago ya Trump ya marekebisho makubwa ya serikali iliyoundwa kuhusiana na malalamiko yake.

Biden alishinda idadi kubwa ya wajumbe na kila hatua ya uteuzi isipokuwa katika hatua moja tu, ambayo ingefanya uteuzi wake kuwa kitu cha kawaida. Hivi sasa kwa vile ameamua kujiondoa, wajumbe hao watakuwa huru kumuunga mkono mgombea mwingine. Nini kitatokea bado hil haliko bayana.

Hatua ya Rais Biden aliyoichukua Jumapili kwa ajili ya kuwania tena kurejea White House, imemaliza ushindani wake na hili kwa kiasi kikubwa linaelezewa linatokana na kutofanya vizuri katika mdahalo wake wa kwanza na Donald Trump na kuongeza mashaka kuhusu hali yake kiafya miezi minne tu kabla ya uchaguzi mkuu.

Uamuzi umekuja baada ya kuongezeka kwa shinikizo kutoka kwa washirika wa Biden katika chama cha Democratic kumtaka ajiondoa kufuatia mdahalo wa Juni 27, ambapo kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 81 hakujieleza vizuri, na mara nyingi hakuwa akitoa majibu yanayoeleweka na kushindwa kuelezea maelezo yasiyo ya kweli ambayo yalitolewa na rais wa zamani.

Mipango ya Biden kuhudumu kwa muda uliobaki madarakani, utamalizika saa sita mchana Januari 20, 2025.

“Imekuwa ni heshima kubwa sana katika maisha yangu kuhusu kama Rais. Wakati ilikuwa azma yangu kuwania kuchaguliwa tena, naamini ni kwa maslahi mazuri ya chama change na nchi yangu kusimama na kujiondoa na kulenga katika kufanikisha wajibu wangu kama Rais kwa muda uliobaki,” Biden aliandika katika barua aliyobandika kwenye akaunti yake katika mtandao wa X.

Biden, ambaye bado yuko nyumbani kwake Delaware baada ya kugundulika ana COVID 19 wiki iliyopita, amesema atazungumza na taifa baadaye wiki hii kutoa “maelezo” kuhusu uamuzi wake.

White House imethibitisha uhalali wa barua hiyo.

Forum

XS
SM
MD
LG