Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Septemba 16, 2024 Local time: 11:40

Mgombea Mwenza wa Trump, JD Vance ajitambulisha


Mgombea mwenza wa Trump, JD Vance akihutubia mkutano wa hadhara huko Youngstown, Ohio, U.S., Septemba 17, 2022. Picha na REUTERS/Gaelen Morse/maktaba
Mgombea mwenza wa Trump, JD Vance akihutubia mkutano wa hadhara huko Youngstown, Ohio, U.S., Septemba 17, 2022. Picha na REUTERS/Gaelen Morse/maktaba

Katika hotuba iliyosubiriwa kwa hamu kubwa na wamarekani, hatimaye JD Vance alisimama mbele ya jukwaa kujitambulisha na kuelezea ajenda za chama cha Republican katika mkutano wa chama cha Republican unaokamilika siku ya Alhamisi huko Milwaukee, Wisconsin.

JD Vance alijitosa kwenye ukumbi wa Fizer kutoa hotuba yake ya Kwanza tangu kuchaguliwa kama mgombea mwenza

Alisema, “Tumeacha kuagiza wafanya kazi kutoka nje ya nchi. Tutapigania raia wa Marekani na kazi zao nzuri na mishahara yao mizuri.”

Akiwa haijulikani kote Marekani, Vance mhitimu wa shule ya Yale Law ambaye alihudumu katika jeshi la Marekani kwa miaka sita -- amehudumu katika ofisi iliyochaguliwa kwa takriban mwaka mmoja na nusu. Alitambulishwa na mkewe, Usha Vance.

"Tumechaguliwa kusaidia kuongoza nchi yetu kupitia baadhi ya changamoto zake kuu. Ninawashukuru nyote kwa imani mliyoweka kwake.” alisema mke wa mgombe mwenza huyo.

Akizungumza Mbele ya umati, wajumbe na wafuasi wa chama, wote walikuwa makini kuona JD Vance ataangazia vipi masuala ya Kigeni ambayo ndiyo kipaumbele ya Marekani.

“Kwa pamoja, tutahakikisha washirika wetu wanashiriki katika kutafuta suluhu ya amani duniani, hakuna msaada ya bure tena kwa mataifa ambayo yanasaliti ukarimu wa walipa kodi wa Marekani." alisema Vance.

Tetesi kuhusu JD Vance hana uzoefu ulipingwa vikali na baadhi ya wajumbe.

Mjumbe kutoka Texas Walter Goodwater, alisema

"Kweli tunachochagua hapa ni uongozi unaowezekana, na amepata uongozi uliothibitishwa, na yeye ni kijana sio kama sisi wazee”

Mwanawe Trump Donald Trump Jr, aliwahimiza wamarekani kupigia chama cha Republican kwani kilenga kuleta mabadiliko makubwa.

“Ni chaguo kati ya wamarekani wanaojivunia na watu wasiopenda Marekani, na mwisho, ni chaguo kati ya Marekani na Marekani kwanza." alisema.

Mkutano huu unakamilika siku ya Alhamis, chaguo sasa linasalia kwa wapiga kura kwa jimbo hili la wisconsin ambalo ni jimbo lenye ushindani mkali iwapo wataipigia kura Republican kwa wingi na pia ilikuwa ni kongamano la kushawishi wa Marekani.

Forum

XS
SM
MD
LG