Rais wa Marekani Joe Biden amekosoa uamuzi wa mahakama ya juu siku ya Jumatatu ambao uliwapa marais kinga pana dhidi ya mashtaka kwa vitendo rasmi vilivyofanywa wakati akiwa madarakani, katika kesi inayohusisha juhudi za rais wa zamani Donald Trump kubadili matokeo ya uchaguzi wa 2020.
Hakuna aliye juu ya sheria, hata Rais wa Marekani, Biden alisema wakati wa hotuba yake kutoka White House Jumatatu jioni. Biden aliapa kuendelea kuheshimu mipaka ya madaraka ya urais lakini alionya kuwa marais wa baadaye hawawezi.
Rais yeyote, akiwemo Donald Trump, sasa atakuwa huru kupuuza sheria, Biden alisema. Rais alisema uamuzi wa Jumatatu ni wa hivi karibuni katika mfululizo wa mashambulizi katika miaka ya karibuni juu ya kanuni mbalimbali za kisheria zilizoanzishwa kwa muda mrefu katika taifa letu na mahakama akitaja maamuzi dhidi ya haki za utoaji mimba na sheria za kupiga kura za kiraia, kati ya maamuzi ambayo yanadhoofisha utawala wa sheria katika taifa hili.
Forum