Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 04, 2024 Local time: 03:21

Mahakama ya Juu ya Marekani yaamua Trump ana kinga ya kiasi


Rais wa zamani wa Marekani Donald akiwa Mahakamani New York, Marekani.
Rais wa zamani wa Marekani Donald akiwa Mahakamani New York, Marekani.

Mahakama ya Juu ya Marekani leo Jumatatu imetoa maamuzi  kuwa rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ana kinga kwa  matendo yoyote rasmi aliyofanya  ya kujaribu kubadili kuchaguliwa kwake tena katika uchaguzi wa mwaka 2020, lakini hana kinga kwa matendo yasiyo rasmi.

Mahakama hiyo imeziachia mahakama za chini kufanya maamuzi ni kesi zipi ambazo Trump anaweza kufunguliwa mashitaka.

Uamuzi huo wa majaji 6 dhidi ya watatu kwenye siku ya mwisho ya muhula wa sasa wa mahakama unamhakikishia Trump kuwa hatashtakiwa katika kesi kabla ya uchaguzi wa Novemba 5 ambapo yeye ni mgombea mteule wa chama cha Republican, anatarajiwa kukabiliana tena na Rais Joe Biden, Mdemocrat aliyemshinda katika uchaguzi wa 2020.

Trump amekanusha kufanya kosa lolote linalohusishwa na matokeo ya uchaguzi wa 2020 lakini kwa muda mrefu amekuwa akidai kulikuwa na matatizo katika upigaji kura na kuhesabu kura ambayo kumemfanya ashindwe kupata muhula mwingine wa miaka minne huko White House.

Kama akishindwa katika uchaguzi wa Novemba, huenda mara tu akakabiliwa na kesi inayohusishwa na uchaguzi wa 2020, lakini kama akishinda, anaweza kumuelekeza mwanasheria mkuu wake, mwendesha mashtaka mkuu wa nchi, kuacha na kesi hiyo.

Mahakama Kuu ilikuwa ya kwanza kufanya maamuzi iwapo rais zamani huenda akashtakiwa kwa kesi ya uhalifu kwa vitendo vyaka alivyofanya wakati akiwa madarakani, au kama ana kinga ya kumzuia kushtakiwa.

Msingi wa sheria za Marekani unaelezea wazi kwamba hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria, kuwa kila mtu ana uhuru sawa lakini pia kila mtu anaweza kushtakiwa kwa kuvunja sheria.

Trump alidai kuwa ana kinga ya kiutendaji, akisema kwamba kumshtaki kwa kujaribu kubadili kushindwa kwake miaka minne iliyopita, alikuwa akichukua hatua kama rais akijaribu kuimarisha uadilifu katika matokeo, akisisitiza kwamba alishindwa kwasababu ya wizi na matatizo mengine katika uchaguzi.

Trump ameshindwa katika dazeni ya kesi mahakamani akidai kuwa aliibiwa katika uchaguzi alipowania awamu ya pili, na mpaka hivi leo mara kwa mara anatoa madai kama hayo ambayo si kweli, na mara chacche akisema ameshindwa kuchaguliwa tena na Biden.

Mwanasheria maalum wa Wizara ya Sheria Jack Smith alimshutumu Trump katika makosa manne yaliyowasilishwa huko Washington karibu mwaka mmoja uliopita kwa njama ya kutaka kubadili mtokeo ya uchaguzi wa 2020, kujihusisha na njama ya kubadili kushindwa kwake ili abakie madarakani.

Forum

XS
SM
MD
LG