Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 05:19

Biden ajiondoa kwenye kinyang'anyiro cha urais Marekani


Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden

Rais wa Marekani Joe Biden Jumapili alitangaza anaondoka kwenye kinyang'anyiro cha urais na kusitisha  kampeni yake ya kutaka kuchaguliwa kwa muhula wa pili.

Hayo yalijiri baada ya wanademokrat wenzake kupoteza imani na uwezo wake wa kumshinda Donald Trump, kufuatia mdahalo kati yake na rais huyo wa zamani, ambaye ni mgombea urais kwa tikiti ya chama cha Republikan.

Biden, katika ujumbe kwenye mtandao wa X, alisema atasalia katika nafasi yake kama rais hadi muhula wake utakapokamilika Januari 2025 na atalihutubia taifa wiki hii.

"Imekuwa heshima kubwa maishani mwangu kuhudumu kama Rais wenu. Na ingawa imekuwa nia yangu kutaka kuchaguliwa tena, naamini ni kwa manufaa ya chama changu na nchi kwa mimi kujiondoa. Nitaendelea kutekeleza majukumu yangu kama Rais kwa muda uliosalia wa muhula wangu," Biden aliandika.

Kwa kutupilia mbali azima yake yakuchaguliwa tena, Biden anamfungulia njia Makamu wa Rais Kamala Harris kugombea katika nafasi ya kwanza, mwanamke wa kwanza Mweusi kufanya hivyo katika historia ya nchi.

Biden, 81, hakumtaja alipotangaza kujiondoa kwake. Haikuwa wazi kama Wademokrat wengine waandamizi wangepingana na Harris kwa uteuzi wa chama, ambaye alionekana kuwa chaguo la maafisa wengi wa chama - au ikiwa chama chenyewe kingechagua kufungua uwanja wa uteuzi.

Sasa, Wanademokrasia wanapaswa kujaribu haraka kuleta mshikamano katika mchakato wa uteuzi katika muda wa wiki chache na kuwashawishi wapiga kura katika muda mfupi sana kwamba mteule wao anaweza kumshinda Trump.

Na kwa upande wake, Trump lazima aelekeze umakini wake kwa mpinzani mpya baada ya miaka ya kuelekeza umakini wake kwa Biden.

Uamuzi huo unaashiria mwisho wa miaka 52 ya harakati za Biden katika siasa za uchaguzi. Biden alishinda idadi kubwa ya wajumbe na kwa kuwa sasa amejiondoa, wajumbe hao watakuwa huru kumuunga mkono mgombea mwingine.

Harris, 59, alionekana kuwa mrithi mtarajiwa kwa sehemu kubwa kwa sababu ndiye mgombea pekee ambaye anaweza kuingia moja kwa moja kwenye nafsi kama hiyo kwa urrahiusi kulingana na sheria za fedha za kampeni ya shirikisho.

Forum

XS
SM
MD
LG