Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 01:16

Vifaa vya kutengenezea bomu vyakutwa nyumbani kwa mtuhumiwa aliyemshambulia Trump


Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akiondolewa jukwaani na Secret Service baada ya shabulizi la risasi. Picha na AP
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akiondolewa jukwaani na Secret Service baada ya shabulizi la risasi. Picha na AP

Vyombo mbalimbali vya usalama vimeharakisha kutafuta majibu siku ya Jumapili, kabla ya siku moja baada ya aliyetaka kuwa muuaji kumfikia karibu na kupiga risasi na kumjeruhi rais wa zamani Donald Trump katika mkutano wa hadhara katika vijiji vya jimbo la Pennsylvania.

Idara mbalimbali za usalama zimezidisha uchunguzi wao kupata majibu siku ya Jumapili, chini ya siku moja baada ya aliyetaka kumuua kumfikia karibu vya kutosha na kumjeruhi rais wa zamani Donald Trump katika mkutano wa hadhara katika vijiji vya jimbo la Pennsylvania.

FBI mapema Jumapili asubuhi wamemtaja mhuhumiwa wa shambulio hilo kuwa Thomas Matthew Crooks mwenye umri wa miaka 20, mkazi wa Bethel Park, Pennsylvania, kilometa 80 kaskazini mwa sehemu ambako mkutano huo ulifanyika huko Butler.

Crooks alipigwa risasi na kuuliwa na Secret Service wa Marekani muda mfupi baada ya kufyatua risasi mfululizo kwa Trump.

Polisi wakivyatua risasi baada ya risasi kuvyatuliwa katika mkutano wa hadhara ambao rais wa zamani Donald Trump alikuwa akihutubia. Picha na AP
Polisi wakivyatua risasi baada ya risasi kuvyatuliwa katika mkutano wa hadhara ambao rais wa zamani Donald Trump alikuwa akihutubia. Picha na AP

Lakini tayari ushahidi mpya unapendekeza tukio hilo lingeweza kuwa baya zaidi.

Maafisa usalama wameliambia Shirika la habari la Associated Press, vifaa vya kutengeneza bomu vimekutwa katika gari la mshukiwa aliyefanya shambulizi katika mkutano wa hadhara wa Trump. Pia vimekutwa vifaa vya kutengenezea bomu nyumbani kwake.

Maafisa wawili ambao hawana mamlaka ya kuzungumza hadharani, walizungumza na The Associated Press wakitaka majina yao yasitajwe.

Shirika hilo pia la habari limeripoti kuwa maafisa wawili wa polisi waliliambia shirika hilo wachunguzi wanaamini silaha ilinunuliwa takribani miezi sita iliyopita na baba wa Thomas Matthew Crooks ambaye ametajwa ndiyo mfyatuaji risasi takriban miezi sita iliyopita.

Maafisa wa serikali bado wanafanyakazi kuelewa lini na jinsi gani Crooks aliweza kupata bunduki na kukusanya taarifa kuhusiana naye wakati wakijaribu kufahamu azma ya shambulio lake.

Secret Service wakimfunika rais wa Zamani Donald Trump baada ya shambulio. Picha na AP
Secret Service wakimfunika rais wa Zamani Donald Trump baada ya shambulio. Picha na AP

Uchunguzi umeelekezwa kwa Crooks. Maafisa hawana mamlaka ya kujadili kwa undani taarifa za uchunguzi na wamezungumza na shirika la habari la AP kwa misingi majina yao yasitajwe.

Wakati huo huo, Pentagon Jumapili imesema ina amini Crooks hana uhusiano na Jeshi la Marekani.

“Tumethibitisha na kila idara ya jeshi hakuna uhusiano na jina la mshukiwa au tarehe ya kuzaliwa katika idara yoyote, wanajeshi waliopo kazini au ambao hawako kazini katika data zao hayumo” kulingana na taarifa kutoka kwa msemaji wa Pentagon Meja Jenerali Pat Ryder.

Shambulio la risasi dhidi ya Trump limelaaniwa na viongozi mbalimbali duniani akiwemo rais wa Marekani Joe biden, Warepublican naWademocrat.

Kupitia mtandao wa X, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ameandika “Jaribio ka kutaka kumuua rais wa zamani Donald J. Trump ni ukumbusho tosha wa hatari ya siasa zenye misimamo mikali na kutovumiliana. Vurugu za kisiasa ni kinyume cha demokrasia, Ninamtakia afueni ya haraka raisi wa zamani Trump. Tunaikemea siasa hii.”

Polisi wakiwa katika eneo ulipofanyika mkutano wa hadhara. Picha na AP
Polisi wakiwa katika eneo ulipofanyika mkutano wa hadhara. Picha na AP

Naye rais wa Nigeria Bola Tinubu ameandika “ Shambulio la rais wa zamani wa Marekani halipendezi na linavuka mipaka ya kanuni za demokrasia. Ghasia hazina nafasi katika demokrasia. Natoa pole kwa rais wa zamani Trump na kumtakia ahueni.

Pia natoa pole kwa familia ya aliyefariki na waliojeruhiwa nawatakia ahueni ya haraka. Nigeria inasimama pamoja na Marekani katika wakati huu”.

Baadhi ya taarifa hizi zinatika shirilka la habari la Associated Press na Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG