Shambulizi hilo lilikuwa moja wapo ya matukio makubwa ya ghasia za kisiasa za Marekani kwa miongo kadhaa.
FBI imesema kuwa Crooks ni kutokea mji wa Bethel Park, Pennsylvania, umbali wa takriban saa moja kutoka kwenye eneo la tukio, ambako Trump alikuwa akihutubia mkutano wa kisiasa.
Taarifa zaidi kuhusu Crooks hazijatolewa, lakini mashuhuda wamesema kuwa alitumibunduki aina ya riffle akiwa kwenye paa ya nyumba nje ya uwanja wa mkutano, kabla ya kuuwawa na mmoja wa maafisa wa usalama.
Idara hiyo imesema kuwa uchunguzi unaendelea kutokana na tukio hilo, na kwamba yeyote mwenye taarifa zaidi anaweza kuziwasilisha.
Mmoja wa watu waliokuwa wakihudhuria mkutano huo alikufa, huku wengine wawili wakijeruhiwa wakati wa mkutano huo iliokuwa akifanyikia eneo wazi karibu na mji wa Butler, Pennsylvania.
Mapema leo Jumapili, mchunguzi maalum wa FBI, ofisi ya Pittsburg, Kevin Rojek ameambia wanahabari kuwa inashangaza kuwa mtu huyo alipiga risasi nne hadi tano kabla ya kupigwa risasi na kuuwawa.
Forum