Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 14:42

Biden alaani vikali shambulizi la bunduki dhidi ya Trump


Rais wa Marekani Joe Biden akizungumza mjini Rehoboath Beach, Delaware, muda mfupi baada ya rais wa zamani na mgombea urais kwa tikiti ya chama cha Republican Donald Trump kushambuliwa kwa risasi.
Rais wa Marekani Joe Biden akizungumza mjini Rehoboath Beach, Delaware, muda mfupi baada ya rais wa zamani na mgombea urais kwa tikiti ya chama cha Republican Donald Trump kushambuliwa kwa risasi.

Rais  Joe Biden alilaani vikali shambulio la kutumia bunduki  dhidi ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akisema kwamba "halikubaliki nchini Marekani".

Tump alipata jeraha kichwani Jumamosi baada ya kufyatuliwa risasi katika mkutano wa kampeni mjini Butler, Pennsylvania.

“Trump ana haki ya kufanya kampeni, na ghasia za kisiasa hazikubaliki Marekani," Biden alisema katika hotuba fupi kwa taifa aliyotoa akiwa mjini Rehoboath Beach, jimbo la Delaware.

Katika taarifa, kampeni ya Trump ilisema mgombea huyo wa urais kwa tikiti ya chama cha Republican alipokea matibabu katika kituo kimoja cha afya, na kwamba “yuko salama”.

Mwendesha mashtaka wa kaunti ya Butler, Richard Goldinger, aliambia shirika la habari la AP kwamba mtu anayeshukiwa kufanya shambulizi hilo alifariki, na kwamba mmoja wa waliokuwa wanahudhuria mkutano huo pia alipoteza maisha yake.

Baadaye, waziri wa usalama wa ndani wa Marekani Alejandro N. Mayorkas alitoa taarifa ifuatayo:

"Mkurugenzi wa Huduma ya ulinzi wa rais, Siri Cheatle, na mimi tumemfahamisha Rais Biden kuhusu ufyatuaji risasi wa leo huko Pennsylvania. Tunashirikiana na vyombo vya usalama ili kujibu na kuchunguza ufyatuaji huo."

"Tunalaani vurugu hizo vikali na tunaipongeza Huduma ya ulizi wa rais kwa hatua yao ya haraka leo. Tunashirikiana na Rais Biden, Rais wa zamani Trump, na kampeni zao, na tunachukua kila hatua inayowezekana ili kuhakikisha usalama wao. Kudumisha usalama wa wagombea Urais na hafla zao za kampeni ni moja ya vipaumbele muhimu vya wizara yetu," aliongeza.

Trump baadaye aliwapongeza maafisa wa usalama kwa "kuchukua hatua za haraka" kufuatia shambulizi hilo na kutuma risala za rambirambi kwa familia ya mtu mmoja aliyepoteza maisha yake katika tukio hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG