Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Agosti 23, 2024 Local time: 05:06

Rais Joe Biden awaomba Wamarekani kupunguza uhasama wa kisiasa baada ya jaribio la mauaji dhidi ya Trump


Rais Joe Biden akilihutubia taifa akiwa katika ofisi yake ya White House, Julai 14, 2024. Picha ya Reuters
Rais Joe Biden akilihutubia taifa akiwa katika ofisi yake ya White House, Julai 14, 2024. Picha ya Reuters

Rais wa Marekani Joe Biden Jumapili amehutubia taifa akiwa katika ofisi yake ya White House akiwataka Wamarekani kupunguza uhasama wa kisiasa na kukumbuka kuwa wote ni majirani baada ya jaribio la mauaji dhidi ya rais wa zamani Donald Trump.

Shambulio la risasi dhidi ya Trump katika mkutano wa kampeni yake huko Pennsylvania siku ya Jumamosi “ inatuomba sote kutafakari,” Biden alisema. Nashuruku Trump hajukujeruhiwa vikali, alisema.

“Hatuwezi kuruhusu ghasia kama hizi kuwa jambo la kawaida.

Kauli za kisiasa katika nchi hii zimekuwa za uchochezi. Ni wakati wa kupoza joto la kisiasa,” alisema.

“Sote tuna jukumu kufanya hivo.”

“Nchini Marekani tunasuluhisha tofauti zetu kwenye sanduku la kura. Hivyo ndivyo tunavyofanya. Kwenye sanduku la kura. Sio kwa risasi,” Biden alisema katika hotuba ya dakika saba, na iliyopeperushwa moja kwa moja na vyombo vikuu vya habari na kituo cha televisheni cha Fox News.

Ilikuwa mara ya tatu Biden kutumia ofisi yake ya White House kuzungumzia masuala nyeti kwa Wamarekani tangu alipoingia madarakani mwaka 2021.

Forum

XS
SM
MD
LG